Pages

Tuesday, December 17, 2013

TANZANITE YAAGWA TAYARI KWENDA AFRIKA KUSINI KURUDIANA NA BASETSANA







TIMU ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ itaondoka kesho kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mechi ya marudiano ya kufunzu kombe la dunia huku ikiwa na matumaini ya kufanya vizuri.

Katika mechi ya kwanza dhidi ya Afrika Kusini iliyochezwa hivi karibuni kwenye uwanja wa nyumbani wa Taifa wa Dar es Salaam, Tanzanite ilichapwa mabao 4-1, hivyo inahitaji kushinda katika mchezo huo kuanzia mabao 5 ili iweze kusonga mbele. 

Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) Boniface Wambura alisema jana kuwa timu hiyo wakiongoza na kiongozi mmoja wa msafara wataondoka kuanzia saa nne na nusu kwa ndege ya Fast Jet.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo wa marudiano Kocha wa Tanzanite Rogasian Kaijage alisema wana matumaini ya kufanya vizuri kwa vile walirekebisha mapungufu yaliyojitokeza katika mechi ya kwanza dhidi ya timu hiyo.

“Mchezo uliopita  ulikuwa na mapungufu kidogo, lakini kwa sasa tumeshayarekebisha na tuna imani ya kufanya vizuri jambo la muhimu ni watanzania kutuombea,”alisema.
Kaijage alisema licha ya kufanya vibaya katika mechi ya kwanza wanahitaji kupewa moyo na sio kulaumiwa kwa kupoteza mchezo mmoja, kwa vile huweza kuwakatisha tamaa wachezaji.

Kwa upande wake, Nahodha wa timu hiyo Fatma Issa aliomba watanzania kuacha kuwakatisha tamaa na badala yake wawape moyo na kuwaombea ili kurudi na ushindi.
Alisema “tunaahidi kufanya vizuri kwasababu tayari Kocha amerekebisha mapungufu, jambo la muhimu nawaomba watuombee,”.

Aliwataka watanzania kutovunjika moyo kwa matokeo mabaya yaliyopita na kuongeza kuwa kutokana na marekebisho makubwa yaliyofanywa wana imani ya kufanya vizuri.

No comments:

Post a Comment