Pages

Sunday, December 29, 2013

AZAM KUONDOKA JANUARI MOSI KWENDA ZANZIBAR KUTETEA KOMBE LA MAPINDUZI



KIKOSI cha Azam FC, kinatarajiwa kuondoka Dar es Salaam Januari mosi, kuelekea visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Akizungumza jijini, Meneja wa Azam FC, Jemadari Said Kazumari,alisema  Azam itaondoka na wachezaji 33 wakiwemo waliopandishwa kutoka timu B na huenda Humphrey Mieno akakosekana kwa vile bado hajawasili kujiunga na mazoezi

“Timu inatarajiwa kuondoka Januari mosi kwenda Zanzibar kuanza kutetea ubingwa wake wa Mapinduzi lakini tunaweza kumkosa Mieno kwani bado hajafika kambini na tumekuwa tukimtumia ujumbe wa barua pepe na sms kumuuliza kulikoni amechelewa, lakini hajibu, hivyo hatuelewi sababu iliyomchelewesha,”alisema.

Jemadari alisema Mieno alipewa ruhusa ya awali lakini ilipomalizika aliwasiliana na uongozi na kusema ana matatizo ya kifamilia, hivyo akaongezewa muda ambao pia umeisha.

Pia Jemadari alisema wana mchezaji mpya mazoezini kutoka Don Bosco ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Djunes Kayanda aliyewahi pia kuchezea Zanaco ya Zambia.

Jemadari amesema mshambuliaji huyo ni kijana mdogo ana umri wa miaka 19 ingawa kwa sasa hawezi kusajiliwa, lakini uongozi umempa muda zaidi kuendelea kuangalia kiwango chake.

Azam ina wachezaji watano wa kigeni, ambao ni kiungo Kipre Balou na washambuliaji Kipre Tchetche na Muamad Ismael Kone wote kutoka Ivory Coast pamoja na Mganda Brian Umony na Mkenya Humphrey Mieno.

Kone amesajiliwa msimu huu kuchukua nafasi ya beki Mkenya, Joackins Atudo aliyemaliza mkataba wake.  
Kikosi kinachotarajiwa kuondoka ni wachezaji; Aishi Manula, Abdallah Karihe, Aggrey Morris, Bryson Nkulula, Brian Umomy, David Mwantika, Erasto Nyoni, Farid Mussa,  Gaudence Mwaikimba, Gadiel Michael, Himid Mao, Ibrahim Mwaipopo na Ismail  Gambo

Wengine ni Jabir Aziz, John Bocco, Joseph Kimwaga, Kelvin Idd, Kipre Tchetche, Kone Ismael Mouhamed, Hamis Mcha, Luckson Jonathan, Bolou Kipre, Malika Ndeule, Mudathir Yahya, Mwadini ali mwadini, Reyna Mgungila, Said Moradi
samih Nuhu, Swalehe Abdallah, Wandwi Jackson, Waziri Salum, Salum Abubakar, Humphrey Mieno na Hamadi Juma 

Wakati viongozi watakaoongozana na timu ni kocha Mkuu Joseph Omog na kocha msaidizi Kalimangonga Ongala, Mwnandi Mwankemwa ambaye ni daktari wa timu, Jemadari Said ambaye ni meneja wa timu.

Viongozi wengine ni Ibrahim Shikanda, Idd Abubakar, Vivek Nagul, Vicent Juma, Twalibu Mbaraka, Yusuf Nzawila na Swalehe Awadh.

No comments:

Post a Comment