Pages

Sunday, December 29, 2013

TAFCA YAWAKUMBUSHA WANACHAMA WAKE KULIPA ADA MAPEMA



WANACHAMA wa Chama cha Makocha Tanzania (TAFCA) wametakiwa kulipa ada za unachama mapema ili kusaidia chama kutekeleza malengo yake kwa wakati.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa TAFCA, Michael Bundala wakati akifanya mahojiano na gazeti hili katika ofisi za chama hicho zilizopo Karume, Dar es Salaam.

Bundala alisema kuwa kwa sasa TAFCA ina wanachama 300 Tanzania nzima na kuwataka makocha wote waliosomea kujiandikisha kwenye ofosi za wilaya na mikoa na kulipa ada ili wawe wanachama hai wapate fursa zinazotolewa na cham,a chao.

“TAFCA tuna wanachama 300 nchini idadi ambayo ni ndogo kulinganisha na idadi ya makocha waliopo nchini ambao tayari wamesomea  hivyo tunawataka kulipa ada ya uanachama ambayo ni 24,000 kwa mwaka”, alisema Bundala.

Bundala alisema asilimia 40 ya ada hiyo inabaki kwenye ofisi za mkoa kusaidia shughuli za ofisi na asilimia 60 inaletwa TAFCA makao makuu.

Pia alisema wana mpango wa kuendeleza mafunzo ya ukocha katika mikoa mipya ili kupata makocha ambao wataendeleza soka katika mikoa hiyo.

No comments:

Post a Comment