Pages

Sunday, December 29, 2013

TIMU SITA ZAFUZU HATUA YA MWISHO LIGI DARAJA LA NNE KILINDI, TANGA



TIMU sita zimefanikiwa kuingia kwenye hatua ya pili ya Ligi daraja la nne wilaya ya Kilindi baada ya kumalizika hatua ya makundi.

Akizungumza na kwa simu toka Kilindi, Katibu wa Chama cha Soka wilaya ya Kilindi, (KDFA), Omari Javu alisema kuwa timu hizo zitaanza kumenyana katika hatua ya mwisho Januari 5, katika Uwanja wa Mabobwe, Songwe mjini.

“Ligi imefikia hatua ya mwisho na jumla ya timu sita zimefanikiwa kuingia hatua hii na zitaanza kuchuana kwenye uwanja wa Mabobwe uliopo Songwe mjini.

Timu zilizotinga hatua hiyo ni Kilindi FC na Dogodogo City toka kundi A la Songe mjini,  Mzalendo FC na Town stars toka kundi B la Mafisa,  Kiting FC  toka kundi C la Kwekwizu na Tingisha FC toka kundi D ambazo zitacheza kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

Ligi hiyo ilianza ikiwa na timu 14  na inachezeshwa na waamuzi waliofuzwa sheria za soka na mkufunzi wa mkoa wa Tanga Damian Mabena.

No comments:

Post a Comment