Pages

Wednesday, November 27, 2013

VAN PERSIE NA VIDIC NJE, KUKOSA MCHEZO WAO NA BAYER LEVERKUSEN LEO

NAHODHA Nemanja Vidic na Robin van Persie wataikosa Mechi ya Manchester United huko BayArena dhidi ya Bayer Leverkusen ya Kundi A la UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI. 

Meneja David Moyes amethibitisha kukosekana kwao na wote hawakuwemo kwenye Kikosi kilichosafiri leo kutoka Jiji la Manchester kwenda huko Germany.
Licha ya Vidic kufanya Mazoezi Asubuhi hii, Moyes amesema: “Wote bado wana maumivu. Wote si maumivu ya muda mrefu lakini hawapo tayari kwa sasa.”
Hata hivyo, Man United itafarijika kwa kurudi tena Kikosini kwa ‘kiraka’ Phil Jones ambae alikuwa nje kwa maumivu ya nyonga lakini itawakosa Michael Carrick, ambae ni Majeruhi, na Marouane Fellaini, ambae yupo Kifungoni kwa Mechi moja baada ya Kadi Nyekundu katika Mechi iliyopita ya Kundi A la UCL walipotoka Sare na Real Sociedad huko Spain. 

Hii ni Mechi ngumu kwenye Kundi A ambayo Mshindi wake ndie atakaefuzu kusonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ingawa kwa Man United hata Sare kwao si mbaya.
Wakiwa kwao BayArena Msimu huu, Bayer Leverkusen wameshinda Mechi zao zote kasoro moja dhidi ya Mabingwa wa Germany na Ulaya, Bayern Munich, ambayo walitoka Sare.

Ryan Giggs ambaye bado anajipa moyo na kuwapa moyo wenzake bado anadai kuwa kuja kufika mwezi wa kwanza watakuwa sehemu yao ya juu kwenye ligi kuu licha ya kufanya vibaya mwanzoni mwa msimu huu.

Baadhi ya wachezaji wa United wakifanya mazoezi kabla ya kuelekea Ujerumani

Giggs akiwekwa kati kwenye mazoezi leo!
Anderson: Majanga wenda akasepa Old Trafford!!Wayne Rooney anaweza kucheza kati lakini kocha wake Moyes anataka acheze mbele!!
Meneja wa United David Moyes anasongwa na wachezaji kadhaa ambao ni majeruhi.

Marouane Fellaini kwenye mazoezi leo hii huku Michael Carrick akiwa anasongwa na majeraha aliyoyapata hivi karibuni.
Katika Mechi ya kwanza iliyochezwa Old Trafford Mwezi Septemba, Man United iliifunga Bayer Leverkusen Bao 4-2.
Katika Mechi ya leo, Man United wanahitaji ushindi ili wafuzu kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL lakini pia hata Sare itawafanikisha.Vile vile, Uwanjani kwao BayArena hawafungiki na mara ya mwisho kufungwa ni Mwezi walipofungwa na Mabingwa Bayern Munich. 
Ashley Young na Jonny Evans kwenye uwanja wa ndege Manchester kabla awajapaa kuelekea Cologne Ujerumani.
MSIMAMO:
KUNDI A
NATIMUPWDLFAGDPTS
1Manchester United42206338
2Bayer 04 Leverkusen42118537
3FC Shakhtar Donetsk412135-25
4Real Sociedad401315-41

No comments:

Post a Comment