Pages

Wednesday, November 6, 2013

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: JUVENTUS YATOKA SARE NA REAL MADRID 2-2, LLORENTE ALAZIMISHA SARE, BALE NA CRISTIANO RONALDO WATUPIA!!


Mkwaju wa penati wa dakika ya 42 kipindi cha kwanza wa dakika za mwishoni unawapeleka mapumziko Juventus wakiwa vifua wazi juu ya Real baada ya Arturo Vidal kuwafungia bao hilo. Ni baada mchezaji Pogba kufanyiwa rafu ndani ya box.

Kipindi cha pili dakika ya 52 Cristiano Ronaldo anaisawazishia bao Real Madrid baada ya kuwatoka mabeki wa Juve na kumchambua kipa kwa kutupia upande wa pili wa kulia na kufunga bao hilo la kusawazisha bao kwa kufanya 1-1 dhidi ya wenyeji Juve.

Bale anaifungia bao la pili Real dakika 60 baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Cristiano Ronaldo na kufanya 2-1.

Dakika ya 65 Llorente anaisawazishia bao Juve kwa kutupia kwa kichwa safi na kumpita kipa wa Real Madrid hadi langoni.


Bale akishangilia baada ya kutupia bao lake kipindi cha pili dakika ya 60 baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Cristiano Ronaldo.

Bale akionesha alama zake kama ishara za ufungaji wake kama kawaida ...furaha baada ya kufunga bao

Cristiano Ronaldo akimfunga kipa wa Juventus Gianluigi Buffon kufanya Real Madrid waongoze kwa 2-1

Ronaldo akishangilia na kupongezwa na wenzie hapa baada ya kusawazisha bao.

Bale na Ronaldo wakikumbatiana kupongezana

Arturo Vidal akimfunga kipa Iker Casillas kwa mkwaju wa penati

Mchezaji wa Juventus Fernando Llorente akifunga bao kwa kichwa na kusawazisha

Llorente akipongezwa na wenzake na mbele ya mashabiki wao Juventus

Luka Modric akimwangusha chini Paul Pogba

Kocha wa timu ya Madrid Carlo Ancelotti akimwangalia kisawasawa Ronaldo akitaka kumtoka Kwadwo Asamoah 

No comments:

Post a Comment