Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, November 12, 2013

LIONEL MESSI NJE MIEZI 2, KUKOSA MICHEZO 8

Mchezaji wa Barcelona Lionel Messi amethibitishwa kuwa itabidi asicheze kwa kipindi cha kati ya Wiki 6 hadi 8 akijiuguza Musuli za Pajani. 

Messi, mwenye Miaka 26, Jana ilibidi atolewe nje kwenye Mechi ya La Liga Barcelona walipoifunga Real Betis Bao 4-1 akiwa na maumivu ya Paja la Mguu wa kushoto. 
Msimu huu, Messi amekuwa akiandamwa na kuumia mara kwa mara na Mwezi Agosti alitolewa kwenye Mechi na Atletico Madrid akiwa na tatizo kama hili la sasa.
Mwezi Septemba, kwenye Mechi na Almeria tatizo hilo hilo likarudi tena.
Leo, Messi alifanyiwa uchunguzi wa kina na ikagundulika kuwa amechanika Musuli ya Paja la Mguu wa Kushoto (Hamstring).
Klabu ya Barcelona imetoa tamko kuthibitisha kuumia kwa Messi na kusema atakuwa nje kwa Wiki 6 hadi 8 na kwanza atatibiwa Mjini Barcelona kisha kurudi kwao Buenos Aires, Argentina kuendelea na matibabu. 

Messi atazikosa Mechi za Kirafiki za Nchi yake Argentina ambazo watacheza katikati ya Mwezi huu na Ecuador na Bosnia-Hercegovina.

Pia Messi atazikosa Mechi za Barcelona za La Liga pamoja na Mechi zao mbili za Kundi lao la UEFA CHAMPIONZ LIGI za kukamilisha Ratiba dhidi ya Ajax na Celtic kwani wameshafuza kuingia Raundi ya Mtoano inayofuata.

Msimu huu Messi amepiga Bao 14 katika Mechi 14 za Barcelona 
 

MITANANGE ATAKAYO KOSA MESSI

Nov 23   Barcelona vs Granada     
Nov 26   Ajax Amsterdam vs Barcelona   
Dec 1     Athletic Bilbao vs Barcelona    
Dec 8     Cartagena vs Barcelona
Dec 11    Barcelona vs Celtic     
Dec 14    Barcelona s Villarreal     
Dec 18    Barcelona vs Cartagena
Dec 22    Getafe  vs Barcelona  

No comments:

Post a Comment