Pages

Sunday, November 17, 2013

KIPA ARSENAL WOJCIECH SZCZESNY ASAINI MKATABA MPYA WA MUDA MREFU NA KLABU YAKE

Kipa Wojciech Szczesny amesaini dili mpya Klabuni kwake Arsenal itakayomweka kwa muda mrefu zaidi. 

Msimu huu, Wojciech Szczesny ameisaidia sana Arsenal kufanya vizuri na hata kuwa inaongoza Ligi Kuu England kitu ambacho kimeleta matumaini kwamba wanaweza kutwaa Ubingwa Msimu huu. 

Akithibitisha habari hizi, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema: “Tumefurahi Wojciech amesaini Mkataba wa muda mrefu. Siku zote nilikuwa naamini yeye ni Mchezaji mwenye Kipaji, mwenye uwezo mzuri na mwenye nguvu kiakili. Anaendelea kukua na kuwa bora zaidi kila wakati. Atakuwa ni sehemu muhimu kwa Arsenal kwa Miaka mingi ijayo.” 


Szczesny, mwenye Miaka 23 na ambae alijiunga na Arsenal Mwaka 2006 akitokea Legia Warsaw ya Poland, amesema: “Nimefurahi sana kusaini Mkataba mpya. Arsenal ni kama Familia yagu na nimefurahi nitabaki hapa kwa muda mrefu.”
Hata hivyo, hakuna alietoboa Dili hiyo ya muda mrefu ni Miaka mingapi.

No comments:

Post a Comment