Lina Kessy (kulia) akiwa na viongozi na wachezaji wa 20 ya wanawake kabla ya kuondoka kwenda Msumbiji |
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Lina Kessy kuwa kamishna wa mechi ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika kwa wanawake chini ya umri wa miaka 20 kati ya Afrika Kusini na Botswana.
Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya kwanza itachezwa nchini Afrika Kusini, Novemba 9 mwaka huu. Waamuzi kutoka Zambia ndiyo watakaochezesha mechi hiyo namba kumi.
Waamuzi hao wataongozwa na Glads lengwe atakayepuliza filimbi wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Bernadette Kwimbira kutoka Malawi, namba mbili ni Mercy Zulu na mezani atakuwepo Sarah Ramadhani, wote wa Zambia.
Afrika Kusini ilishinda mechi ya kwanza ugenini mabao 5-2. Mshindi wa mechi hiyo atacheza raundi ya pili na mshindi wa mechi kati ya Tanzania na Msumbiji.
No comments:
Post a Comment