Pages

Sunday, November 17, 2013

AZAM YAANZA KWA KICHAPO UHAI CUP, MAKAMU WA RAIS TFF, WALES KARIA AFUNGUA ASHUKURU UDHAMINI WA UHAI

Kamisaa wa mchezo, Joseph Kanakamfumu akimpokea Makamu wa Rais wa TFF Wales Karia na viongozi mbali mbali kwa ajili ya kusalimiana na wachezaji

Makamu wa Rais wa TFF Wales Karia akisalimiana na waamuzi

Makamu wa Rais wa TFF Wales Karia akisalimiana na wachezaji wa Azam FC

Makamu wa Rais wa TFF Wales Karia akisalimiana na wachezaji wa Coastal Union

Makamu wa Rais wa TFF Wales Karia akisema neno kuashiria ufunguzi wa mashindano

Waamuzi na timu wanapiga kura kuchagua timu ya kuanza mchezo

Benchi la Azam FC 

Benchi la Coastal Union

Viongozi wakifuatilia mpambano

Wachezaji wa Azam FC wakishangilia bao

Wachezaji wa Coastal Union

"Unipiti kirahisi wewe"



Kocha wa Coastal Union Mkenya Yusuph Chiko
TIMU ya Azam Fc inayoshiriki michuano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 (U20) kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom leo imeanza vibaya mashindano hayo baada ya kufungwa mabao 2-1 na Coastal Union ya Tanga.

Azam ambao walikuwa wa kwanza kupata bao kwenye dakika ya tatu kupitia kwa mshambuliaji Eric Haule baada ya kuwazidi mbio mabeki wa Coastal Union, bao ambalo lilidimu kwa kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu kufanya mabadiliko, hali iliyofanya mchezo kubadilika na kushambuliana kwa zamu lakini zamu hii Coastal waliizidi Azam Fc kila sehemu.

Iliichukua Coastal Union dakika tano (daakika ya 50) kwenye kipindi cha pili kusawazisha bao kupitia kwa kiungo mshambuliaji Raizin Haji kwa njia ya penati baada ya beki wa Azam Fc kunawa mpira eneo la hatari.

Dakika tano baadae (dakika ya 55) Raizin Haji aliifungia Coastal bao la pili baada ya kuwapiga chenga mabeki wa Azam hadi golikipa na kutia mpira wavuni kirahisi na kuamsha nderemo na vifigo kwa mashabiki waliokuwa wamefurika uwanjani hapo.

Baada ya matokeo hayo Azam walionekana kuchoka na kushindwa kuhimili mashambulizi ya Coastal lakini shukrani kwa mlinda mlango wao Hamadi Juma kwani alijitahidi kuokoa michomo mingi licha ya kufungwa hayo mabao mawili.

Awali akifungua mashindano hayo Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF) Wales Karia alishukuru udhamini wa maji ya Uhai kwani umesaidia kuibua vipaji na kusema TFF ina mikakati ya kuongeza mashindano mengi ya kuhusisha umri ukiacha yale ya U-15 yanayodhaminiwa na Coca cola.

“Nashukuru udhamini wa maji ya Uhai kwani vijana wanatakiwa wacheze mara kwa mara ili kusaidia kuinua vipaji ambavyo vitakuwa hazina kwa taifa hapo baadae”, alisema Karia.

No comments:

Post a Comment