Pages

Monday, November 18, 2013

KIINGILIO CHA KUISHANGILIA STARS 5,000/-


Kiingilio katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya wenyeji Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe ni sh. 5,000 kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Mbali ya kiingilio hicho cha sh. 5,000 ambacho ni kwa viti vya bluu na kijani, viingilio vingine ni sh. 30,000 kwa VIP A, sh. 20,000 kwa VIP B, sh. 15,000 kwa VIP C wakati viti vya rangi ya chungwa ni sh. 10,000.

Tiketi zitauzwa katika magari maalumu katika vituo vya; Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Ohio na Samora, Sokoni Kariakoo, Dar Live Mbagala, OilCom Ubungo, BMM Salon iliyopo Sinza Madukani, Uwanja wa Uhuru, mgahawa wa Brake Point uliopo Kijitonyama, na kituo cha mafuta Buguruni.

No comments:

Post a Comment