Pages

Thursday, October 24, 2013

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: MANCHESTER UNITED 1 vs REAL SOCIEDAD 0

Manchester United wanapata bao dakika ya pili baada ya Rooney kuachia shuti kali na kugonga posti na hatimaye mchezaji wa Real Sociedad Iñigo Martínez anajifunga kwa kuokolea ndani. mpaka Hafu taimu timu ya Manchester ndio imeenda ikiongozwa kwa bao hilo la mapema la kujifunga huku United wakicheza vizuri karibu kipindi chote cha dakika za kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili pamoja na United kukosa nafasi nyingi za kufunga timu zote zimetoka ya bila kufungana kipindi hicho cha pili, dakika 90 zikimalizika kwa bao hilo moja la kujifunga.
Mchezaji wa  Real Sociedad Inigo Martinez akijifunga  hapa baada ya presha kubwa ya washambuliaji wa United moja wapo aikiwa Rooney na Chicharito walianzishwa mbele kwa ushambuliaji huo.Baooo..  Wachezaji wa Manchester United wakishangilia kwa kupongezana apaMchezaji hatari wa  Manchester United Wayne Rooney (nyuma) na wa  Real Sociedad Inigo Martinez wakigombea mpira hapa kipindi cha kwanzaWazee wazima nao walikuwemo kushoto ni Kocha wa zamani wa   Manchester United  Sir Alex Ferguson akiteta na  Chief Executive David Gill....usipime!!
Sehemu maalumu iliyotengwa eneo la Jukwaa likiwa limetengwa maalum kwa ajili ya Washabiki 1,400 ambao kazi yao ni kuimba Nyimbo ili kuhamasisha timu yao ya United.


RATIBA/MATOKEO
Jumatano 23 Oct 2013

Bayer 04 Leverkusen 4 v Shakhtar Donetsk 0
Manchester United 1 v Real Sociedad 0

Real Madrid 2 v Juventus 1
Galatasaray 3 v København 1
RSC Anderlecht 0 v Paris Saint-Germain 5
SL Benfica 1 v Olympiacos FC 1
FC Bayern München 5 v FC Viktoria Plzeň 0
CSKA Moscow 1 v Manchester City 2

No comments:

Post a Comment