Pages

Thursday, October 24, 2013

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: ANDERLECHT 0 vs PARIS SAINT-GERMAIN 5, ZLATAN IBRAHIMOVIC APIGA HAT-TRICK NA EDISON CAVANI WAKIIUA ANDERLECHT KWAO!!

Paris Saint-Germain wakiwa ugenini wakikaribishwa na kucheza klabu bingwa Ulaya ni timu ya Anderlecht wamechinjwa chinjwa na kikosi cha PSG bao tano bila kujitetea.
Huku Mchezaji Zlatan Ibrahimovic akitupia bao zake tatu peke yake ikiwa ni hat-trick bao hizo zikifatana dakika ya 17,22, na 36 katika kipindi cha kwanza. Bao la nne limefungwa dakika ya 52 na mchezaji hatari tena Edinson Cavani na la tano likifungwa tena na Zlatan Ibrahimovic katika dakika ya 62. Magoli hayo yametosha kumaliza mchezo huo huku
Anderlecht wakitoka patupu bila ya bao la kufutia machozi kwenye uwanja wao. Ushindi huo unawaweka juu wakiwa na pointi 9 na magoli 11.


Mchezaji wa Paris Saint-Germain Zlatan Ibrahimovic, (kati), akipongezwa baada ya kuiua hat-trick Anderlecht
Ibrahimovic akishangilia

Kipa wa Anderlecht Thomas Kaminski akipimiwa na Ibrahimovic

Ibrahimovic akiongoza mpira hapa

Edinson Cavani kaziona nyavu mara moja za Anderlecht
RATIBA/MATOKEO
Jumatano 23 Oct 2013

Bayer 04 Leverkusen 4 v Shakhtar Donetsk 0
Manchester United 1 v Real Sociedad 0

Real Madrid 2 v Juventus 1
Galatasaray 3 v København 1
RSC Anderlecht 0 v Paris Saint-Germain 5
SL Benfica 1 v Olympiacos FC 1
FC Bayern München 5 v FC Viktoria Plzeň 0
CSKA Moscow 1 v Manchester City 2

No comments:

Post a Comment