Pages

Wednesday, October 23, 2013

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: ARSENAL 1 v BORUSSIA DORTMUND 2


Gunners wako wakicheza kwenye uwanja wao wa Emirates Stadium kwa kuwakaribisha Borussia Dortmund wameanza vyema kipindi cha kwanza baada ya kufungwa bao na wao kusawazisha bao hilo kipindi cha kwanza. Arsenal ndio walianza kufungwa na mchezaji wa Borussia Dortmund Henrikh Mkhitaryan  dakika ya 16 kwa shuti kali baada ya mchezaji wa Gunners kujichanganya na kutokwa mpira. Baadae dakika ya 41 Olivier Giroud akawasawazishia bao hilo na kufanya 1-1 kipindi cha kwanza nacho kikaisha. Henrikh Mkhitaryan akipewa pasi safi kutoka kwa  Robert Lewandowski  na kutofanya makosa na kuifunga  Arsenal
Wachezaji wa  Borussia Dortmund wakipongezana baada  Mkhitaryan kuwapa bao la mapema

No comments:

Post a Comment