Pages

Tuesday, October 22, 2013

FULHAM ILIPOIFUMUA CRYSTAL PALACE 4-1 KATIKA MCHEZO WA ENGLISH PREMIER LEAGUE NYUMBANI KWAO

Crystal Palace wakiwaalika wenzao Fulham kwenye uwaja wao Selhurst Park kucheza mchezo wa kuhitimisha ratiba ya raundi ya nane kwenye ligi kuu England. Wakiongozwa na refa Lee Mason. Kumbuka mtanange huu timu zote mbili zinajikongoja kutoka chini ili ziweze kupanda juu, Fulham wapo nafasi ya 17 na Crystal Palace wapo nafasi ya 19 na wakiwa wamekalia kuti kavu nyuma yao kuna timu inayoshikilia kuti hilo Sunderland ambao walifungwa bao 4 juzi.
Mchezaji wa Crystal Palace Mariappa ndio ameanza kuifungia timu yake dakika ya 7 kabla ya Kasami wa Fulham kusawazisha bao hilo katika dakika ya 19.
Dakika za mwisho kipindi cha kwanza dakika ya 45 Fulham walipiga frii kiki na ukuta wa Crystal Palace wakazuia na mchezaji wa Fulham Sidwel akamalizia mpira huo kwa shuti kali mpaka langoni mwa lango la Crystal na kipa wao kutoona ndani na mpira kumalizika kipindi cha kwanza Fulham wakiongoza kwa 2-1dhidi ya wenyeji.
Kipindi cha pili dakika ya 50 Krosi safi kama kona na Dimitar Babatov akaunganishia nyavuni kwa ndoo na kuandika bao la tatu. 
Kipindi cha pili hicho hicho dakika 55 Mchezaji Senderos aliyeingia kipindi cha pili akatupia tena bao la nne huku kipa akiuokolea ndani ya lango lake.  Steve Sidwell akichongaa bao hapa mwishoni mwa kipindi cha kwanza
Kasami na Sidwell wakipongezana hapa baada ya kuifungia bao Fulham usiku huu.
Mmiliki wa  Fulham  Shahid Khan nae akatupia tano juu!!Dimitar Berbatov akitupia kwa kichwa hapaBerbatov akishangilia bao lakePhilippe Seneros (nyuma) akishangilia baada ya kufunga baoWafungaji wa Fulham Kasami, Sidwell na Berbatov wakifurahia pamoja Wachezaji wa Fulham wakishangilia na kupongezana

No comments:

Post a Comment