Pages

Monday, September 2, 2013

WENGER ALEMEWA, ATAKA KUFANYA KILA KITI ARSENAL


London, England
LICHA ya Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kukubali kwamba mchakato wa usajili ni tatizo kwake, ameonesha kiburi na ubinafsi mkubwa, baada ya kusisitiza kwamba kamwe hatakubali kufanya kazi chini ya mkurugenzi wa soka.

Tottenham ambayo jana iliwavaa wapinzani wao hao wa London, 'The Gunners’, yenyewe ilimteua Franco Baldini kama mkurugenzi wa soka majira haya ya joto na kisha kumpa Muitalia huyo jukumu zima la mchakato wa usajili.

Matokeo yake ni Spurs kufanikiwa kuvunja rekodi yake ya usajili, kwa kusaini nyota bora ikijiandaa kumkosa Gareth Bale.

Lakini Arsenal imeshindwa kufanikiwa kuipata saini ya Luis Suarez na Wayne Rooney, huku ikifanikiwa tu kuwasajili kwa uhamisho huru Yaya Sanogo na Mathieu Flamini kuelekea dirisha la usajili linalofungwa leo saa sita usiku.

“Siwezi kufanya kazi chini ya mkurugenzi wa soka kwa sababu wananunua wachezaji na wanaposhindwa kucheza vema, unalaumiwa kwa kutowatumia ipasavyo,” alisema Wenger.

“Sipingi kutokuwa na mtu wa kunisaidia kununua, kuuza na kufanya mazungumzo, kwa sababu sitaweza kufanya kila kitu. Lakini nadhani uamuzi wa mwisho mara zote lazima ubaki kwa kocha kuamua nani asajiliwe na yupi auzwe kwa kuwa yeye ndiye muwajibikaji kwa staili ya uchezaji na matokeo.”

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, huko England, Wenger aliongeza: “Ni kama kuandika makala yako na mtu fulani aseme nitabadilisha hiki na hiki. Hutaweza kukubaliana na hilo, simamia kile ulichokiandika! Ninasimamia matokeo ya timu niliyoichagua. Kocha lazima awajibike kwa wachezaji wanaosajiliwa.”

Lakini Wenger alipoulizwa kuwa anabeba mzigo mkubwa sana kwa kujaribu kuiandaa timu na kuhusika moja kwa moja katika usajili, Mfaransa huyo, 63, alikubali kuwa inaweza kuwa ngumu.

“Siwezi kukataa kuwa mchakato wa usajili ni tatizo kwangu, kwa sababu unaingia kwenye mzozo wakati mashindano tayari yameshaanza na ninahitaji kuelekeza nguvu katika mashindano.

“Si rahisi tena kwa sababu soko la kimataifa lipo wazi zaidi. Kuna washindani wengi lakini wachezaji ni wachache. Mara zote ninahitaji kuwa katika nafasi ambayo sina wakununua. Ndiyo maana nina watu wanaonizunguka kunisaidia, lakini uamuzi wa mwisho lazima hutokea kwa kocha.”

No comments:

Post a Comment