Pages

Monday, September 2, 2013

PELLEGRINI: CITY ITATINGA MTOANO UEFA, MOURIHNO: BADO JEMBE MOJA NA TEVEZ AZIDI KUINOGESHA JUVENTUS



 Manchester, England
KOCHA mpya wa Manchester City, Manuel Pellegrini anaamini kuwa, kwa mara ya kwanza atafanikiwa kuivusha timu hiyo kwenye hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kwa misimu miwili iliyopita, City imeshindwa kuvuka hatua ya makundi licha ya kutumia kitita kikubwa katika usajili.

Hata hivyo, katika michuano ya msimu huu hatua ya makundi, licha ya kupanga pamoja na bingwa mtetezi Bayern Munich, pamoja na CSKA Moscow na Viktoria Plzen ya Czech, Pellegrini amejigamba kuivusha miamba hiyo ya Etihad.

Akijivunia historia yake ya msimu uliopita ya kuivusha Malaga hatua ya mtoano, Pellegrini alisema: "Labda timu moja inaweza kuwa na historia kuliko nyingine kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini ninauhakika msimu uliopita wakati Milan ilipojua kuwa ipo kundi moja na Malaga walifurahia kwa kuwa tulikuwa dhaifu, ila tulijipanga na kisha kuvuka."

@@@@@@@@@

Mourinho: Bado jembe moja

London: KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho licha ya kufanikiwa kumsajili Samuel Eto'o kutoka Anzi, bado anahitaji mshambuliaji mmoja kabla ya dirisha la usajili kufungwa leo usiku.

Taarifa zimeeleza kuwa, Mourinho anataka kurejea maombi yake aliyoyatoa kwa Mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Robert Lewandowski wakati akiwa Real Madrid, sambamba na kujaribu bahati kwa Karim Benzema.

@@@@@@@@@

Tevez azidi kuinogesha Juventus

Milan: MSHAMBULIAJI mpya wa Juventus, Carlos Tevez amefunga mechi tatu mfululizo alizocheza Serie A, ambapo juzi alikamilisha idadi hiyo kwa kucheka na nyavu mara moja, wakati  mabingwa hao wa Italia wakiibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Lazio.

Arturo Vidal ndiye aliyefunga mabao mawili ya awali, huku Miroslav Klose akifanikiwa kupunguza idadi hiyo ya mabao kwa upande wa Lazio, kabla ya Mirko Vucinic kutupia la tatu huku Tevez akihitimisha ushindi huo kwa kufunga la nne.

No comments:

Post a Comment