Pages

Monday, September 2, 2013

USAIN BOLT AMJIA JUU MOYES, STOKE YAMALIZANA NA ARNAUTOVIC NA CHELSEA YAMNASA 'MESSI WA GHANA'



Usain Bolt amjia juu Moyes
MANCHESTER, England
KICHAPO cha bao 1-0 ambacho Manchester United ilikipata kutoka kwa Liverpool kimemkera bingwa wa mbio fupi duniani, Usain Bolt, ambaye alimjia juu kocha wa United, David Moyes na kumwambia timu bado sana.
Kwa kutumia akaunti yake ya Instagram, Bolt aliweka video ambayo alijirekodi akifoka kwa kusema; “Mimi ni Usain Bolt na ni shabiki mkubwa wa Manchester United. David Moyes, tunahitaji kiungo mbunifu anayejua kupiga pasi na kutengeneza nafasi sasa!”

@@@@
Stoke yamalizana na Arnautovic
STOKE, England
STOKE City imekamilisha usajili wa straika wa Werder Bremen, Marko Arnautovic (24), kwa ada ya pauni milioni 2 na kumpa mkataba wa miaka minne, huyu ni mchezaji wa nne kusajiliwa na Mark Hughes, baada ya ujio wa Erik Pieters, Marc Muniesa na Oussama Assaidi.
Katika hatua nyingine, West Bromwich Albion jana ilifanikiwa kumnasa kiungo Morgan Amalfitano (28), kutoka Olympic Marseille ya Ufaransa. 

@@@
Chelsea yamnasa ‘Messi wa Ghana’
LONDON, England
CHELSEA wamekamilisha usajili wa Lionel Messi wa Ghana, Christian Atsu (21) kutoka Porto kwa dau la pauni milioni 3.5 juzi na kumsainisha mkataba wa miaka mitano, lakini kinda huyo amepelekwa kwa mkopo Vitesse Arnhem ya Uholanzi.
Atsu, ambaye msimu uliopita aliichezea Porto jumla ya mechi 17 kati ya hizo nane kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, amekuwa akijulikana kwa jina la utani la Messi wa Ghana.

No comments:

Post a Comment