Pages

Monday, September 2, 2013

ROONEY, PHIL JONES, JOHNSON WATEMWA ENGLAND, MAN CITY YAMNASA DEMICHELIS, KAKA ARUDI RASMI MILAN NA SAKHO, ILORI, MOSES WATUA LIVERPOOL




LONDON, England
KOCHA wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson, ana wakati mgumu kuelekea kwenye mechi za kimataifa za kuwania kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Moldova na Ukraine, Ijumaa na Jumanne hii, kutokana na majeruhi kuiandama timu yake.
Wayne Rooney, Phil Jones na Glen Johnson watakosa mechi hizo muhimu kwa England katika harakati zake za kusaka tiketi za kushiriki michuano ya Kombe la Dunia mwakani, nchini Brazil. Rooney anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu kutokana na majeraha ya kichwa.

@@@@
Man City yamnasa Demichelis
MANCHESTER, England
KLABU ya Manchester City imethibitisha kunasa saini ya beki wa kati wa Atletico Madrid, Martin Demichelis (32) kwa dau la pauni milioni 3.5 na kumpa mkataba wa miaka miwili.
Demichelis ametua City ili kuongeza nguvu kwenye beki ya timu hiyo na usajili wake unaifanya Man City kutumia zaidi ya pauni milioni 100 wakati huu wa usajili, baada ya kuwanasa mastaa wengine kama kina Fernandinho, Jesus Navas, Alvaro Negredo na Stevan Jovetic wakati huu Manuel Pellegrini akijipanga kutengeneza timu yake.
 @@@@
 
Kaka arudi rasmi Milan
MILAN, Italia
HATIMAYE klabu ya AC Milan imetangaza kupitia mtandao wake kwamba imefanikiwa kumrudisha nyumbani kiungo wake wa zamani, Ricardo Kaka (31), kutoka Real Madrid na imemsainisha mkataba wa miaka miwili ambao utamuweka San Siro hadi 2015.
Baada ya mazungumzo marefu asubuhi ya jana jijini Madrid, kati ya Adriano Galliani na wawakilishi wa Kaka, walikubaliana Mbrazil huyo ataingiza kiasi cha euro milioni 4 kwa msimu, Kaka anarudi kwenye timu aliyoichezea  kati ya mwaka 2003 – 2009.
@@@@
 
Sakho, Ilori, Moses watua rasmi Liverpool
LIVERPOOL, England
KLABU ya Liverpool imeendelea kuimarisha kikosi chake, baada ya jana kukamilisha usajili wa mabeki wawili, Mreno Tiago Ilori (20), kutoka Sporting Lisbon, pamoja na Mfaransa Mamadou Sakho (23) kutoka Paris Saint Germain.
Ilori ametua Liverpool kwa dau la pauni milioni 8 na Sakho kwa dau la pauni milioni 16, pia jana walikamilisha usajili wa mkopo wa Victor Moses kutoka Chelsea na kuungana na Kolo Toure, Iago Aspas, Luis Alberto, Simon Mignolet na Aly Cissokho, mastaa ambao wametua Anfield wakati huu wa kiangazi.

No comments:

Post a Comment