Pages

Sunday, September 1, 2013

TORRES NA MATA WATEMWA TIMU YA TAIFA

MADRID, Hispania
KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya Hispania, Vicente Del Bosque, amewaengua washambuliaji wawili wa Chelsea, Fernando Torres na Juan Mata, katika kikosi chake kinachojiandaa na mechi ya kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Finland na ile ya kimataifa dhidi ya Chile.

Washambuliaji hao wawili walikuwemo kwenye kikosi cha timu hiyo kilichotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini na ule wa Ulaya, lakini wanakumbana na wakati mgumu kwenye klabu yao ya London.

Torres, 29, anabaki kuwa kama mchezaji kivuli tofauti alivyokuwa Liverpool na licha ya kufunga bao la kwanza juzi katika mechi ya Super Cup juzi dhidi ya Batern Munich katika matokeo ya 2-2, bado alitolewa nje huku Mata, 25 akijikuta akiwekwa kando na kocha Jose Mourinho kwenye mechi muhimu kama hiyo.

Del Bosque amewajumuisha washambuliaji David Villa, Pedro, Roberto Soldado na Alvaro Negredo, pamoja na wenzake na Negredo kwenye kikosi cha Manchester City, David Silva na Jesus Navas.

Hispania inataka kuendelea kuilinda pointi yake moja inayowazidi Ufaransa, ikiwa kileleni mwa kundi I.
Kikosi cha Hispania kitakuwa; Makipa: Iker Casillas (Real Madrid), Victor Valdes (Barcelona) na Pepe Reina (Napoli).

Mabeki: Alvaro Arbeloa (Real Madrid), Sergio Ramos (Real Madrid), Jordi Alba (Barcelona), Raul Albiol (Napoli), Inigo Martinez (Real Sociedad) na Nacho Monreal (Arsenal).

Viungo: Andres Iniesta (Barcelona), Santi Cazorla (Arsenal), Isco (Real Madrid), Koke (Atletico Madrid), Xavi (Barcelona), Mario Suarez (Atletico Madrid) na Sergio Busquets (Barcelona).

Washambuliaji: Jesus Navas (Manchester City), David Silva (Manchester City), Alvaro Negredo (Manchester City), Roberto Soldado (Tottenham Hotspur), Cesc Fabregas (Barcelona), Pedro (Barcelona) na David Villa (Atletico Madrid).

No comments:

Post a Comment