Pages

Sunday, September 1, 2013

ADIDAS WAMZAWADIA BALE VIATU

MADRID, Hispania
WADHAMINI wa viatu vya kiungo mshambuliaji Gareth Bale, kampuni ya Adidas, haikutaka kupoteza muda zaidi ya kutanguliza viatu vipya kwa ajili ya mchezaji huyo, atakavyovitumia katika mazoezi na mechi kwenye kikosi chake kipya cha Real Madrid.

Adidas alifanya utaratibu huo tangu juzi Ijumaa, huku hatua za mwisho za makubaliano zikiwa hazijakamilika vizuri.
Mtandao wa gazeti la michezo la AS uliweka picha kwenye mtandao, ikimuonesha mwakilishi wa kampuni hiyo akipeleka boksi kubwa ambalo inadaiwa kuwa ndani yake kulikuwa na viatu vya Bale ambavyo angekabidhiwa kwenye mazoezi ya timu hiyo.

Pia picha hiyo ilionyesha mojawapo ya kiatu kikiwa kimeandikwa jina la Bale, huku makaratasi ya kupokelea mzigo pia yakiwa na jina la mchezaji huyoa raia wa Wales.
Bale mwenyewe alitarajiwa kutua rasmi Madrid jana Jumamosi, baada ya pande hizo mbili kukubaliana.

No comments:

Post a Comment