Pages

Monday, September 2, 2013

ROBBEN AACHA MAJANGA BAYERN NA JUAN MATA KUAMKIA ARSENAL




epa_soccer_2013-08_2013-08-30_2013-08-30-03844222_epa
Munich, Ujerumani
 Bayern Munich imepata majanga, baada ya mechi ya Ijumaa ya Uefa Super Cup dhidi ya Chelsea, kuibuka mabingwa huku ikiwapoteza wachezaji wake nyota watatu kutokana na kuwa majeruhi.

Viungo Arjen Robben, Javi Martinez na Mario Gotze wote hawataweza kujifua na wenzao wiki ijayo, huku Mjerumani Gotze akielezwa kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu.

Mchezaji wa Kimataifa wa Hispania, Martinez ambaye aliifungia Bayern bao la pili la kusawazisha kwenye mechi hiyo, atayakosa mazoezi kwa muda wa siku tano zijazo kutokana na maumivu ya goti.

Daktari wa timu, Hans-Wilhelm Muller-Wohlfahrt pia aliagiza Robben, ambaye katika mechi hiyo alitolewa dakika ya sita ya muda wa nyongeza kutokana na maumivu ya goti, kupewa muda wa mapumziko.

@@@@@@@@@

Juan Mata kuamkia Arsenal
London, England

Juan Mata leo itamlazimu kulazimisha kuomba kuondoka, ili kumwezesha kuamkia Arsenal kesho, anaripoti Dave Kidd wa Gazeti la Sunday People.

Wiki iliyopita, Sunday People Sport, lilieleza kutambua kuwa 'The Gunners' inataka kumsajili nyota huyo raia wa Hispania, anayeichezea Chelsea na Jumanne Arsene Wenger kuthibitisha hilo.

Lakini Mata anakabiliwa na wakati mgumu kwa kutambua kuwa hataweza kupata nafasi ya kuanza mara kwa mara katika Kikosi cha Chelsea chini ya Jose Mourinho, huku akijua pia hataweza kuuzwa kabla ya dirisha la usajili la majira haya ya joto kufungwa.

Mata, 25, ni kipenzi kikubwa cha mashabiki wa wakali hao wa Stamford Bridge, lakini Mourinho ameweka bayana kuwa Oscar na Eden Hazard moja kwa moja watakuwa chaguo lake la kwanza katika safu ya viungo watatu washambuliaji.

Mhispania huyo aliwekwa benchi wakati 'The Blues'  ikiukosa ubingwa wa Super Cup dhidi ya Bayern Munich Ijumaa.

Katika Kikosi cha Hispania kilichoitwa kujiandaa na mechi za kuwania kufuzu Kombe la Dunia, Mata hakujumuishwa, lakini lengo lake ni kuona akishiriki fainali hizo nchini Brazil majira ya joto yajayo.

Hivyo, wakati huu ambao Arsenal imeonesha nia yake ya kumsajili kwa pauni milioni 30 (sh. bilioni 62.7 za Tanzania), Mata atalazimika kuomba kuondoka ili kuweza kuamkia Emirates kesho kabla ya dirisha la usajili kufungwa leo saa sita usiku.

No comments:

Post a Comment