Pages

Monday, September 2, 2013

LIVERPOOL KUMTANGAZA SAKHO LEO NA FELLAINI KUFUNGA USAJILI UNITED




Liverpool, England
KLABU ya Liverpool jana ilitarajiwa kutangaza mabeki wapya wawili.

Gazeti la The Mail on Sunday, limeeleza kuwa mlinzi wa Paris Saint-Germain, Mamadou Sakho na beki mwenzake wa kati Tiago Ilori wa Sporting Lisbon, Jumamosi walitua Uwanja wa mazoezi wa Liverpool wa Melwood kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya zao.

Wachezaji hao wote kwa pamoja ada yao ya uhamisho inaelezwa kuwa ni jumla ya pauni 23 sawa na shilingi bilioni 48 za Tanzania.




Fellaini kufunga usajili United

Manchester: KOCHA wa Man United, David Moyes ana majina matano mkononi ambayo baadhi yao atafunga nayo ukurasa kabla ya dirisha la usajili la majira haya ya joto kufungwa leo saa sita usiku.

Kiungo wa Everton, Marouane Fellaini leo anatarajiwa kujifunga rasmi United, huyo akiwa ni mmoja kati ya watano wanaowindwa. Wengine ni nyota wa
Borussia Dortmund, Ilkay Gundogan na wa Real Madrid, Luka Modric, Ander Herrera (Athletic Bilbao) na Daniele De Rossi (Roma).


No comments:

Post a Comment