Pages

Monday, September 2, 2013

ILALA YATOKA SARE NA UNGUJA KASKAZINI, COPA COCACOLA


TIMU ya soka ya mkoa wa Ilala leo imetoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya mkoa wa Kaskazini Unguja katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Copa Cocacola uliochezwa kwenye uwanja wa shirika la elimu Kibaha, Pwani.

Timu ya Ilala ndio ilikuwa ya kwanza kuona lango la wapinzani wao katika dakika ya 10 kupitia kwa mshambulaji wake Ally Shabani baada ya kuwazidi mbio mabeki wa Kaskazini Unguja na dakika 35 Ally alifunga bao la pili .

Kipindi cha pili kikianza Ilala wakiwa mbele kwa bao 2-0 lakini Unguja Kaskazini walifanya shambulizi na kufanikiwa kupata bao kupitia kwa Usi  Makame dakika ya 49 kwa penati baada ya beki Jamal Akida kunawa mpira katika harakati za kuondoa mpira eneo la hatari.

Baada ya hapo Ilala walijitahidi kuongeza bao na dakika ya 49 kupitia kwa mshambuliaji wake Harun Said.
Katika dakika ya 64 Shaban Ada wa Ilala  alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumkwatua Faki Juma wa Unguja Kaskazini.

Baada ya kadi nyekundu, Unguja Kaskazini  walizinduka na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya  64 kupitia kwa Jecha Juma.

Unguja Kaskazini waliendelea kuliandama lango la Ilala na dakika 78 walipata penati baada ya  Jamal Akida wa Ilala kumkwatua Haji Makame na Jecha Juma kufunga bao la tatu na kufanya matokeo kuwa 3-3

Mchezo huo ambao ulichezeshwa na Ahmad Seif wa Pwani ulikuwa wa ushindani kwani kila mchezaji alijitahidi kuonyesha uwezo wake na kusaidia timu yake kushinda.

No comments:

Post a Comment