Pages

Monday, September 2, 2013

TIMU YA KMKM YA ZANZIBAR YATWAA NGAO YA JAMII!!


 Timu ya KMKM ya Kisiwani Pemba ikifurahia ushindi wake wa Ngao ya Jamii,mara baara ya kuifunga timu ya Chuoni mabao 5-4 yaliyopatikana kwa mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika tisini ya mchezo kwa kufunguma bao 1-1.Mchezo huo ulipigwa jana usiku kwenye Uwanja wa Gombani,Pemba ikiwa ni sehemu ya ufunguzi wa Ligi kuu ya Grand Malt,Zanzibar.
Mgeni Rasmi katika Mchezo huo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Grand Malt Zanzibar na kuwaniwa kwa Ngao ya Jamii,Waziri wa Serikali ya Mapinduzi asiekuwa na Wizara Maalum,Mh. Haji Faki Shaali (wa pili kushoto) akikabidhi Ngao ya Jami.
Kikosi cha timu ya KMKM
Kikosi cha timu ya Chuoni FC
Beki wa timu ya Chuoni FC akijaribu kumtoka mchezaji wa KMKM
Habari kwa Hisani ya MUHIDIN MICHUZI at MICHUZI BLOG 

No comments:

Post a Comment