Pages

Monday, September 2, 2013

LIVERPOOL NOMA, YAIFUNGA MAN UNITED 1-0

Liverpool's Daniel Sturridge
Wachezaji wa Liverpool wakishangilia bao la Daniel Sturridge lililoipa ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester United kwenye Uwanja wa Anfield. Huo ni ushindi wa tatu mfululizo kwa Liverpool tangu kuanza kwa msimu, matokeo iliyowahi kupata miaka 19 iliyopita. (Picha kwa Hisani ya Gazeti la Daily Mail la Uingereza)Flying start: Daniel Sturridge gave Liverpool the lead with a header in the fourth minute
Sturridge akishangilia bao pekee la Liverpool, alilofunga leo. Ushindi huo umekuja wakati ambao mshambuliaji huyu anaadhimisha miaka 24 ya kuzaliwa kwake leo Septemba 1.
Right place: Sturridge flicked home Daniel Agger's header from two yards
Sturridge akidondoka baada ya kupiga kichwa kufunga bao hilo akiunganisha pasi ya kichwa ya Daniel Agger aliyeunganisha kona ya Steven Gerrard.
On form: Sturridge has scored in all four of Liverpool's matches this season
Embrace: Sturridge hugs manager Brendan Rodgers after giving Liverpool the lead
Sturridge akikumbatiana na kocha wa Liverpool Brendan Rodgers baada ya kuifungia timu yake bao la ushindi.
Stunning: Liverpool fans at the Kop End made a stunning mosaic in honour of Bill Shankly before kick-off
Mashabiki wa Liverpool wakiwa wamekaa jukwaani kuunda picha na kuandika namba 100 ambayo ini idadi ya miaka ambayo nguli wa zamani aliyezaliwa Septemba 2, Bill Shankly ilikuwa aitimize, ingawa alifariki kabla.
Birthday: Players and fans took part in a minute's applause for Shankly a day before he would have turned 100
Fiesty: Steven Gerrard and Robin van Persie share their thoughts with each other
Steven Gerrard wa Liverpool, akitunishiana msuli na Robin van Persie wa Man United wakati wa mechi hiyo.


Physical: Martin Skrtel, who replaced the injured Kolo Toure, rises high to win a header
Martin Skrtel (37), ambaye aliingia kujaza pengo la majeryhi Kolo Toure, akiruka juu kuwania kupiga mpira wa kichwa kuondoa hatari langoni mwa Liverpool.
Effort: Gerrard attempts a shot on goal from a free-kick, which was saved by David de Gea 
Steven Gerrard akipiga adhabu ndogo.
Spectator: England manager Roy Hodgson was in the stands for the clash at Anfield
Kocha wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson (wa pili kulia) akifuatilia mtanange huo wa kukata na shoka kwenye dimba la Anfield.
Sidelined: Liverpool's suspended striker watches the action at Anfield on Sunday
Mshambuliaji Luis Suarez wa Liverpool, akiangalia mechi hiyo akiwa jukwaani.
In the dugout: Liverpool manager Rodgers (right) and Manchester United boss David Moyes
 Kocha wa Liverpool, Rodgers (kulia) na wa Manchester United David Moyes wakitoa maelekeo kwa wachezaji wa vikosi vyao.


BAO pekee la Daniel Sturridge ambaye jana alikuwa akisherekea siku yake ya kuzaliwa lilitosha kuipa Liverpool ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Manchester United kwenye mchezo mkali uliopigwa katika uwanja wa Anfield.

Straika huyo wa kimataifa wa England aliupalaza kidogo mpira wa kichwa ambao ulikuwa umepigwa na Daniel Agger na kuwapita David de Gea na Tom Cleverley waliokuwa kwenye mstari wa goli mapema katika kipindi cha kwanza.

Man United walijaribu kuchomoa bao hilo bila mafanikio, huku Simon Mignolet akionyesha kiwango safi na kufanikiwa kucheza mechi yake ya tatu msimu huu bila kuruhusu bao.
Brendan Rodgers alilazimika kubadilisha kikosi chake cha Liverpool kwa mara ya kwanza msimu huu, kwa kumuweka benchi Kolo Toure ambaye ni majeruhi na nafasi yake kuchukuliwa na Martin Skrtel ambaye alicheza sambamba Daniel Agger.

Wayne Rooney alikosekana kwa upande wa Man United kutokana na majeraha ya kichwa aliyonayo, huku Antonio Valencia pia akianzia benchi na nafasi zao kuchukuliwa na Ashley Young na Ryan Giggs.
Wachezaji wapya wa Liverpool, Tiago Ilori, Mamadou Sakho na Victor Moses wote walikuwa jukwaani kuangalia pambano hilo ambapo timu yao ilianza vizuri na kuandika bao la mapema katika dakika ya nne tu ya mchezo.

Baada ya bao la Liverpool, United walijaribu kusaka bao la kusawazisha lakini Danny Welbeck na Robin van Persie hawakuwa makini na kukosa mabao matatu ya wazi na mpaka pambano hilo linamalizika Liverpool 1, Man United 0.

Katika mchezo mwingine Arsenal waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tottenham Hotspur kwenye pambano kali lililopigwa katika dimba la Emirates.
Olivier Giroud ndiye alikuwa mfungaji wa bao pekee la mchezo huo katika kipindi cha kwanza akimalizia krosi safi ya chini chini iliyopigwa na Theo Walcott kutoka winga ya kulia.
Spurs walijaribu bila mafanikio kuchomoa bao hilo katika kipindi cha pili huku wakitawala sehemu kubwa ya mchezo huo.

No comments:

Post a Comment