Pages

Sunday, September 1, 2013

NI VITA KATI YA LIVERPOOLvs MAN UNITED NA ARSENAL vs TOTTENHAM


LONDON, England
KWA lugha rahisi, unaweza kusema kuwa siku ya leo mtoto hatumwi sokoni.

Usemii huu utadhihirika leo wakati miamba ya soka nchini England, Manchester United na Liverpool, itakaposhuka uwanjani kuumana, zikiwania pointi tatu muhimu kwenye michuano ya Ligi Kuu ya England.

Mbali na timu hizo, pia kuna mtihani mwingine kwa Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, ambaye kibarua chake kipo shakani, baada ya kulazimishwa kusajili wachezaji wapya, lakini yeye akaamua kuweka njiti masikioni.

Mechi hizo zote ni muhimu kwa kila timu kutokana na kuwa ndizo zitakazotoa mwelekeo wa kila timu katika michuano ya  mwaka huu. Kwa mujibu wa historia ya timu hizo,  Liverpool FC na –Manchester United FC, ni timu zenye ushindani mkubwa katika soka la England na pia timu hizo mbili ni kati ya timu zenye mafanikio makubwa kwenye michuano hiyo, zikiwa zimefanikiwa kutwaa mataji  121,  59 yakiwa ni ya  Liverpool na  62 ya  Manchester United.

Ukiachilia mbali ushindani viwanjani, timu zote mbili ni kati ya timu zinazoingiza kipato kikubwa na pia ni timu ambazo zina mashabiki wengi kwenye ulimwengu wa soka.





Viwango vya timu: Man United itakwenda kukikabili kikosi hicho cha Merseyside, ikiwa na kumbukumbu ya Jumatatu ilipotoka sare na mahasimu wao, Chelsea, katika mtanange uliopigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford, mechi ambayo ilikuwa mtihani wa kwanza mkubwa kwenye utawala wa David Moyes.

Matokeo hayo yalikuja ikiwa ni baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Swansea City na mabingwa hao wa msimu uliopita watakuwa wakitaka kurudia rekodi hiyo watakaposhuka kwenye dimba hilo la  Anfield, licha ya jambo hilo kuonekana halitakuwa rahisi kwa timu kama Liverpool, ambayo imeshajikusanyia pointi nzuri kutoka kwenye mechi dhidi ya  Stoke City na Aston Villa, zilizoifanya kuwa moja kati ya timu mbili zilizokwishajiwekea rekodi kwenye Ligi Kuu hiyo ya Barclays.

*Ndani na Nje: Katika mtanange huo, Wayne Rooney anaweza kurejea kwenye nafasi yake ya kuanza kikosi cha kwanza, baada ya Jumatatu kuonesha kiwango kizuri na huku  Ashley Young naye akitarajia kuwamo kikosini.
Kwa upande wao,  Rafael na Javier Hernandez wao bado hawataonekana uwanjani kutokana na kuwa bado ni majeruhi na huku Nani naye akionekana kuwa huenda akaikosa mechi hiyo.

Kwa upande wake Liverpool, Martin Skrtel, anaweza kuwemo uwanjani, lakini kikosi hicho cha Brendan Rodgers kitakuwa hakina wachezaj kama vile  Kolo Toure, Joe Allen na Aly Cissokho, ambao waliumia wakati wa mechi ya Kombe la Ligi  iliyopigwa Jumanne wii hii dhidi ya timu ya Notts County.

*Kivutio
Kivutio katika mchezo huo kitakuwa ni mfungaji bora wa mwaka jana, Robin Van Persie, ambaye mabao yake yaliisaidia klabu hiyo ya Old Trafford kutwaa ubingwa msimu uliopita, huku Liverpool ikimkosa nyota wake, Luis Suares ambaye amefungiwa.

Msimu huu tayari Van Persie ndiye aliyefunga bao la kwanza kabla ya kuunganisha pande alilotengewa na Nemanja Vidic, kabla ya timu hizo kenda mapumziko  wakati, Daniel Sturridge naye akitarajia kuonesha uwezo wake.



*Nyota wa mechi: Baada ya kujiunga na Liverpool akitokea  Chelsea mapema Januari mwaka huu, Daniel Sturridge alijidhihirisha kuwa mmoja wa silaha za maangamizi baada ya kuifungia mabao 12 dakika za mwisho msimu uliopita.
Na katika mwendelezo huo nyota huyo aliyekulia kwenye timu ya watoto ya  Manchester City msimu huu, ameshafunga mabao manne katika mechi tatu alizokwishacheza msimu huu.

Kutokana na hali hiyo, inaelezwa kuwa  mabeki wa Manchester United ni lazima wahakikishe wanamchunga vilivyo mshambuliaji huyo.
*Wachezaji wanavyosema
Kwa upande wa wawachezaji, beki wa Manchester United, Rio Ferdinand, anasema kuwa anaihofia safu ya ushambuliaji ya Liverpool, inayoundwa na wachezaji Danny Sturrrige na Philippe Countino.

Nadhani ni wachezaji wazuri waliosajiliwa mwishoni mwa msimu uliopita. Daniel Sturridge anaonekana kuwa ni mchezaji hatari na Philippe Countino ni mchezaji mzuri,” alisema beki huyo.


*Makocha: Kwa upande wa makocha, Brendan Rodgers ana uhakika vijana wake hawataathirika na dakika 120 walizocheza Jumanne wakati Man Uted itakapowatembelea leo.

 “Tumewapa muda wa kutosha wa kupumzika wachezaji,” aliiambia tovuti ya Liverpool. “Haya ndiyo mawazo ya kwamba nitawatumia baadhi ya wachezaji wakongwe kutokana na kwamba kutakuwepo na ushindani, lakini na kwa kuwachezesha wachezaji vijana kutawasaidia kuwajengea uwezo wa kucheza kwenye mechi zenye ushindani,” alisema kocha huyo, mara baada ya mechi hiyo ya Kombe la Ligi.

Alisema hadi kufikia mtanange wa leo tayari wachezaji wake watakuwa wamepumzika na hivyo atakuwa amejiandaa vilivyo kuwakabili wapinzani wake.

Wakati Rodgers akijitapa hivyo, kwa upande wa Man United, kocha wa zamani wa Everton kwa uzoefu wake wa miaka 11 akiwa na timu hiyo, David Moyes, anazifahamu vilivyo mechi zinazozikutanisha timu hizo na kwamba raia huyo wa Scotland ataingia uwanjani akiwa hana hofu kubwa kuhusu mechi hiyo.



*Waamuzi: Andre Marriner, ndiye atakayekuwa katikati ya dimba  hilo la Anfield.
Mara ya mwisho mashabiki wa Manchester United kumuona ilikuwa ni Machi mwaka huu, wakati timu yao ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Reading katika mechi za Kombe la FA.
Kivutio kwa mwamuzi huyo ni pale msimu uliopita alipowazawadia kadi nyekundu wachezaji watano.

*Mechi tano za mwisho zilizozikutanisha timu hizo


 



15 Oktoba  2011
Liverpool
1-      1
Manchester United     
Anfield,   Ligi Kuu

28 Januari  2012
Liverpool
2–1
Manchester United
Anfield    Kombe la FA

11 Februari 2012
Manchester United
2–1
Liverpool
Old Trafford, Ligi Kuu

23 Septemba 2012
Liverpool
1–2
Manchester United
  Anfield,Ligi Kuu

13 Januari 2013
Manchester United
2–1
Liverpool      Old , Trafford
Ligi Kuu

 

 

 

 

 

*Arsenal v Tottenham Hotspur:

 

Wakati roho za mashabiki  wa Liverpool na Man United zikiwapaa, mvutano mwingine utakuwa ni kati ya Tottenhm na Arsenal ambao utapigwa kwenye uwanja wa  Emirates muda wa saa 10 kwa saa za England.

 

 

 

 

 *Vikosi, Arsenal ambayo huenda ikatumia mfumo wa , 4-2-3-1 huenda ikawatumia wachezaji kama  Szczesny; Sagna, Koscielny, Mertesacker, Gibbs; Ramsey, Wilshere; Walcott, Rosicky, Cazorla; Giroud.

Wakati  Arteta, Diaby, Oxlade-Chamberlain, Podolski na  Vermaelen hawatakuwamo uwanjani kutokana na kuwa majeruhi.

Tottenhma, 4-2-3-1): Lloris; Walker, Dawson, Vertonghen, Rose; Capoue, Paulinho; Townsend, Dembélé, Chadli; Soldado.

Wakati Bale, Lennon, Assou-Ekotto, Adebayor hawatacheza kutokana na hali zao kiafya.

*Mwamuzi  wa pambano hilo atakuwa ni  Michael Oliver.

 

*Habari za timu.

 

Inaelezwa kuwa  licha ya macho yote kuwa uwanjani kwa muda wa dakika zote 90 za mchezo huo, lakini akili zote zitakuwa ni kuhusu usajili  wa Arsenal, baada ya timu hiyo kushindwa kutoa fedha kusajili mchezaji yoyote.

 

 

Hali hiyo inadaiwa kuwa italifanya benchi la ufundi la Arsenal kukaa tumbo joto kutokana na kwamba wanakutana na  Tottenham ambayo ina kikosi kigumu.


*Historia ya hivi karibuni
Nyumbani  21-10,Ugenini 12-5,Sare  13-5.
*Mechi tano za mwisho kukutana Emirates.

Katika mechi hizo tano za mwisho  zilizoikutanisha miamba hiyo zilizalisha mabao 30.

No comments:

Post a Comment