Pages

Monday, August 19, 2013

ALICHOSEMA MZEE WENGER BAADA YA KICHAPO CHA 3-1 KUTOKA ASTON VILLA

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ambae Timu yake ilizomewa baada ya Mechi kwisha:

"Tulianza vyema lakini baada ya hapo kila kitu kilienda ovyo! Kuumia, maamuzi, kucheza Mtu 10 na kukosa nafasi za wazi! Ni Siku mbaya, si kwa kosa ubora, ila kila kitu kilikuwa ovyo dhidi yetu! Sina furaha na ile Penati ya pili lakini kitu ambacho hakinifurahishi zaidi ni jinsi Refa alivyoachia Gemu iende.Nimeshangazwa! Si kazi yangu kuzungumzia sana hilo, ni wajibu wangu kuiangalia Timu yangu.Kitu kinachoniuma ni kuwaangusha Watu wanaoipenda Klabu hii. Nipo hapa kuwafurahisha Watu na kama sitimizi hilo inabidi niombe radhi na nirudi tena na kuwafurahisha katika Gemu nyingine. Tungeweza kushinda Gemu hii na Wachezaji tuliokuwa nao, hilo nina hakika nalo!”Mzee Wenger akiangalia timu yake uwanjani huku mambo yakiwa magum, Jana jioni. 

No comments:

Post a Comment