Pages

Saturday, August 17, 2013

AFRICA YATIA FORA MBIO FUPI KWA WANAWAKE NCHINI URUSI


Mbio fupi za wanawake zimeingia katika zama mpya mara baada ya waafrika wawili raia wa nchi za Cote d'Ivoire na Nigeria kulishindia bara hilo medali kwa mara ya kwanza katika historia, kwenye fainali za mashindano ya dunia ya mita 200 kwa wanawake huko Moscow Urusi jana Ijumaa.

Murielle Ahoure raia wa Cote d,Ivoire mwenye umri wa miaka 25 amejishindia medali ya shaba kwa mara ya pili katika mashindano hayo ya dunia akiweka rekodi ya kuwa mwafrika wa kwanza mwanamke kushinda medali katika fainali ya mbo za mita 100 akifuatiwa na Blessing Okagbare kutoka Nigeria.


Wanawake hao kwa pamoja wamekuwa wakiishii Marekani ingawa asili yao ni Afrika na wamesema kuwa ushindi wao unawakilisha wanawake wa Afrika yote .

No comments:

Post a Comment