Pages

Saturday, August 17, 2013

YANGA YATWAA NGAO YA JAMII BAADA YA KUIFUNGA AZAM FC BAO 1

Wachezaji wa Yanga wakiiibusu ngao ya jamii waliyotwaa baada ya kuifunga Azam bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa leo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadiq Mecky akimkabidhi Nahodha wa Yanga ngao ya jamii baada ya kuifunga Azam FC bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Taifa leo




Mechi ya Ngao ya jamii kuashiria kufungiliwa kwa pazia la ligi kuu soka Tanzania bara baina ya mabingwa watetezi klabu ya Yanga dhidi ya  Azam fc zote za jijini Dar es salaam katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam zimemalizika kwa wanajangwani kuwafunga wapinzani wao bao 1-0 lililofungwa na Salum Telela katika dakika ya 2 ya mchezo akiunganisha krosi safi ya Didier Kavumbagu.

 Kipindi cha pili Yanga walicheza vizuri zaidi na kupata nafasi, lakini kipa kinda wa Azam c, Aishi Manula alikuwa kikwazo kutokana na kuwa imara zaidi katika mchezo huo.
Nao Azam walipata nafasi kadhaa za kufunga, lakini washambuliaji wao wakiongozwa na John Bocco “Adebayor” walishindwa kukabili nafasi hizo kuwa magoli. 


Kabla ya mechi hiyo tambo zilitawala kwa mashabiki wa tmu hizo, huku mashabiki wa Simba wakiishangila Azam kwa nguvu zote, lakini mashabiki wa Yanga walionekana kuwa na matumaini ya ushindi kwani walifika kwa wingi sana uwanjani na mwisho wa mchezo huo wametoka na vicheko.

Azam fc walikuwa Afrika kusini kujiandaa na mechi za ligi kuu Tanzania bara pamoja na huu wa leo ambao wamepoteza kwa kipigo hicho cha bao la mapema la Telela aliyecheza vizuri zaidi katika mchezo wa leo na kama angekuwa makini basi angeifungia timu yake mabao zaidi.
 

Kikosi cha Yanga SC leo kilikuwa: Ally Mustafa ‘Barthez’/Deo Munishi ‘Dida’ dk15, Juma Abdul, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan/Mbuyu Twite dk15, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Salum Telela, Jerry Tegete/Hussein Javu dk 68, Didier Kavumbangu na Haruna Niyonzima.

Kikosi cha Azam FC: Aishi Manula, Erasto Nyoni/Joackins Atudo dk 46, Waziri Salum, David Mwantika, Aggrey Morris, Himid Mao, Kipre Tchetche, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco ‘Adebayor’/Gaudence Mwaikimba dk 74, Kipre Balou/Ibrahim Mwaipopo dk 62 na Khamis Mcha.

 
 

No comments:

Post a Comment