Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara timu ya Young Africans imetoka suluhu ya bila kufungana na timu ya Rhino Rangers katika mchezo uliofanyika jioni hii katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa washabiki.
Young Africans ambayo ilikua ikicheza mchezo wake wa mwisho baada ya kucheza michezo miwili ya awali dhidi ya timu ya Express ya kutoka nchini Uganda ambapo ilitoka sare mchezo mmoja na kufungwa mmoja.
Jerson Tegeta aliipatia Young Africans bao dakika ya kwanza ya mchezo lakini katika hali ya kutatanisha mwamuzi wa mchezo huo alikataa bao hilo hali iliyowafanya washabiki waliofurika katika uwanja huo kumzomea mwamuzi.
Rhino Rangers iliyopanda ligi kuu msimu huu ilifanya mabadiliko haraka haraka katika dakika 30 za mwanzo ambapo ilikua imezidiwa sehemu ya kiungo pamoja na mabadiliko hayo bado vijana wa jangwani waliendelea kuutawala mchezo huo.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans 0 - 0 Rhino Rangers.Kpindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ambapo Young Africans ilimtoa kiungo Hamis Thabit na nafasi yake ikichukuliwa na Abdallah Mnguli ambaye alisaidia kuongeza kasi ya mashambulizi.
Mipira miwili iliyorushwa na mlinzi Mbuyu nusura iipatie Young Africans bao lakini kutokua makini kwa washambuliaji wake kuliwafanya kupoteza nasi hizo za wazi.Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 0 - 0 Rhino Rangers.
Young Africans: 1.Deogratius Munishi 'Dida', 2.Juma Abdul, 3.Oscar Joshua, 4.Mbuyu Twite, 5.Rajab Zahir/Ibrahim Job, 6.Salum Telela, 7.Nizar Khalfani, 8.Hamis Thabit/Abdallah Mnguli, 9.Didier Kavumbagu, 10.Jerson Tegete/Shaban Kondo, 11.Said Bahanuzi
No comments:
Post a Comment