Timu ya Taifa ya
Tanzania (Taifa Stars) inaondoka Mwanza keshokutwa (Julai 24 mwaka huu) kwenda
Kampala, Uganda kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la CHAN itakayochezwa
Jumamosi (Julai 27 mwaka huu) Uwanja wa Mandela kuanzia saa 10 kamili jioni.
Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Mwanza chini ya
Kocha Kim Poulsen tangu Julai 14 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo itakayoamua
ni timu ipi kati ya hizo mbili itacheza Fainali za CHAN zitakazofanyika mwakani
nchini Afrika Kusini.
Timu hiyo itaondoka
Uwanja wa Ndege wa Mwanza saa 7.25 mchana kwa ndege ya PrecisionAir, na
inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 10.15 jioni.
Wakati huo huo, Kocha
Kim Poulsen kesho (Julai 23 mwaka huu) atakuwa na mkutano na waandishi wa
habari kuzungumzia maandalizi ya kikosi chake. Mkutano huo utafanyika saa 5
kamili asubuhi kwenye hoteli ya La Kairo jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment