MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Senegal, Papiss Cisse anaweza kulazimika kuitema klabu ya Newcastle United kwasababu ya sakata la mdhamini mpya wa klabu hiyo ambayo ni kampuni ya mikopo ya Wonga. Nyota huyo ambaye anakadiriwa kulipwa kitita cha paundi 40,000 kwa wiki, alikuwa akifanya mazoezi mwenyewe baada ya kurejea kutoka katika mapumziko ya kiangazi wiki iliyopita baada ya kukataa kuvaa fulana yenye nembo ya mdhamini huyo kwasababu ni kinyume na imani ya dini yake ya Kiislamu.Chini ya Sharia za Kiislamu, muumini yoyote wa dini hiyo hatakiwi kunufaika na fedha za mikopo, huku riba zikiwa hazitolewi katika benki za kiislamu.
Mshambuliaji wa zamani wa West Ham United, Frederic Kanoute ambaye pia ni Muislamu aliruhusiwa na klabu ya Sevilla ya nchini Hispania kufanya fulana isiyokuwa na nembo yoyote wakati klabu hiyo ikidhaminiwa na kampuni ya kamari ya 888.com.
No comments:
Post a Comment