MSHAMBULIAJI wa zamani wa
klabu ya Chelsea, Didier Drogba ametangaza kujenga hospitali tano nchini
kwake Ivory Coast ili kuhudumia afya ya mama na mtoto.Taarifa hizo zilitolewa na
katibu muhtasi wa Mfuko wa Didier Drogba, Guy Roland Tanoh jijini Abidjan mapema
wiki hii. Tanoh amesema kiasi cha dola milioni tano zinatarajiwa kuwekwa katika
mradi huo, huku kila hospitali ikijengwa katika miji mitano mikubwa ya nchi hiyo
ambayo ni Abidjan, Yamoussoukro, Man, Korhogo na San Pedro.Tanoh amesema shughuli kwa
ajili ya kuchangisha kiasi cha dola milioni 4 inatarajiwa kufanyika jijini
London, Uingereza huku kiasi cha dola milioni moja kilichobakia kikitolewa na
Drogba mwenyewe katika kuufanya mradi huo uwe wa kweli.
No comments:
Post a Comment