Pages

Tuesday, June 4, 2013

ST.GEORGE IMEKUWA TIMU YA KWANZA KUTOKA ETHIOPIA KUTINGA HATUA YA MAKUNDI YA KOMBE LA SHIRIKISHO

 
St George imefanikiwa kuwa timu ya kwanza kutoka Ethiopia kufuzu kwa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika licha ya hapo jana kupata kichapo kutoka kwa ENPPI ya Misri.

ENPPI ilishinda katika mchezo huo wa mkondo wa pili kwa bao 3-1 matokeo ambayo yalifanya matokeo ya jumla kusimama kuwa sare ya 3-3 lakini timu hiyo ya Ethiopia imefanikiwa kusonga mbele kwa faida ya sheria ya kupata bao la ugenini.

St George itaungana na Stade Malien ya Mali, Enugu Rangers ya Nigeria na Etoile du Sahel ya Tunisia katika kundi A la michuano hiyo.
Mabingwa wa Algerian Entente Setif, TP Mazembe ya DR Congo, FUS Rabat ya Morocco na CA Bizertin ya Tunisia zote zilipata ushindi katika michezo yao na sasa zinajumuika katika kundi B.

Mshambuliaji raia wa Ivory Coast Vincent Die Foneye alifunga bao la uongozi kwa wenyeji ENPPI baada ya dakika 25 za mchezo lakini Tesfaye Alebachew aliwapa wenyeji wakati mgumu kufuatia kusawazisha bao hilo dakika 12 baadaye.
Die Foneye kwa mara nyingine tena akaandika mabao yake mawili kwa kwa ENPPI katika dakika sita za mwisho na kundika “hat-trick” lakini haikufua dafu hivyo St George ikafuzu.

Stade Malien imeichapa Lydia LB Academic ya Burundi kwa bao 1-0 na kuandika ushindi wa jumla wa mabao 6-0.
Mabingwa mara mbili wa zamani CS Sfaxien wameondolewa mashindanoni kufuatia sare ya bila kufungana na Enugu Rangers ya Nigeria ambao wamepita kwa ushindi wa jumla wa bao 1-0.

FUS Rabat wenyewe wamefanikiwa kusonga mbele baada ya sare ya mabao 3-3 wa Rabat derby dhidi ya FAR Rabat hapo jana na hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3.
Mchezaji wa zamani wa Hibernian Abdesselam Benjelloun aliwapa FUS bao la uongozi dakika tatu yan mchezo kabla ya Mustapha El Yousfi kusawazisha dakika 30 baadaye.
FAR wakaandika bao linguine la pili kupitia kwa Mustapha Allaoui kunako dakika ya 60 lakini mabao mawili ndani ya dakika tatu kupitia kwa Hicham Laroui na Benjelloun yakawapa uongozi FUS tena.

Hata hivyo dakika ya mwisho Youness Hammal akaandika bao la kusawazisha kwa wanajeshi hao na kusonga mbele.
Kulikuwa na taarifa mbaya kwa waarabu wengine wa Misri Ismaili ambao wametolewa mashindano licha ya ushindi wa nyumbani wa bao 1-0 dhidi ya CA Bizertin Tunisia.
Watunisia hao wamesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabaoa 3-1 baada ya ushindi wa mchezo wa kwanza wa mabao 3-0.

TP Mazembe ya DR Congo, chini ya Patrice Carteron pia imesonga mbele  licha ya kichapo cha mabao 2-1 toka kwa Liga Muculmana ya Mozambique.

No comments:

Post a Comment