Pages

Tuesday, June 4, 2013

ETO'O ATAKIWA KUPUMZIKA KWA WIKI KADHAA HUKU TAIFA LAKE LIKIKABILIWA NA MECHI MUHIMU

Timu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi imeliandikia barua shirikisho la soka la Cameroon kutaka nchi hiyo isimtumie Samuel Eto'o katika michezo ijayo ya kampeni ya kuwania kufuzu kombe la dunia  mwaka 2014.

Mtaalamu wa mambo ya tiba za viungo wa klabu hiyo physiotherapist, Stijn Vandenbroucke, amesema mshambuliaji huyo yuko katika maumivu ya msuli aliyoyapata katika mchezo wa fainali ya Russian Cup.

Katika taarifa yao wamesema mshambuliaji huyo anatakiwa kupumzika kwa wiki chache.
Eto'o anatarajiwa kuwasili nchini Cameroon hii leo ili kwamba timu ya waangalizi wa afya ya Indomitable Lion nayo iweze kumfanyia uchunguzi.

Hata hivyo daktari wa timu ya Cameroon ndiye mwenye kauli ya mwisho ya kuamua kama Eto'o yuko fiti ama laa na kama ataweza kutumika katika mchezo wa June 9 dhidi ya Togo na mchezo mwingine dhidi ya DR Congo wiko moja baadaye.

Cameroon wanaongoza kundi I wakiwa na alama sita ikiwa mbele kwa alama moja dhidi ya Libya huku DR Congo ikiwa na alama nne na Togo ikiwa na alama moja.

No comments:

Post a Comment