Pages

Saturday, June 1, 2013

SERIKALI YAOMBOLEZA KIFO CHA MSANII MANGWEA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO 


 SALAAM ZA RAMBIRAMBI KUTOKANA NA KIFO CHA
BW. ALBERT MANGWEA, (Man Ngwair)
1/06/2013.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, imepokea kwa mshituko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva) Albert Mangwea, aliyefariki huko Afrika  Kusini katika hospitali ya St. Hellen akiwa katika shughuli za muziki, Jumanne  tarehe 28 Mei, 2013.

Kifo cha Albert Mangwea ni pigo kubwa kwa fani ya muziki hapa nchini, na pia kimataifa. Na kutokana na umahiri wake katika fani hiyo ya muziki wa kizazi kipya hususan aina yake ya uimbaji ya “Free Style” alikonga mioyo ya wapenzi wake hasa vijana ndani na nje ya nchi.

Albert Mangwea atakumbukwa na wasanii na wapenzi wa muziki  kwa kipaji na juhudi zake za kukuza muziki hapa nchini.

 Serikali inawapa pole ndugu na jamaa wote  na kuwaomba wawe na uvumilivu na subira katika kipindi cha msiba.

Wito wa Serikali kwa wasanii na wananchi kwa ujumla ni kuendelea kumuenzi kwa  yale yote mazuri aliyoyafanya wakati wa uhai wake.

“Mwenyenzi Mungu ailaze roho ya Albert Mangwea mahala pema peponi.”

 Imetolewa na Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara

No comments:

Post a Comment