Pages

Saturday, June 1, 2013

MEMBE ASEMA DARFUR SI SALAMA KWA MASHINDANO YA CECAFA



Waziri wa Mambo ya nje Bernad Camilius Membe amelishangaa Baraza la Vama vya Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) linaloongozwa na Rais wa TFF anayemaliza muda wake,  Leodgar Chila Tenga kwa kupeleka mashindanohayo Sudan Kusini hasa katika jimbo la Darfur kuwa ni bado hali ya usalama si nzuri.

Membe aliyasema hayo wakati akijibu swali lililoulizwa na mbunge katika majadiliano ya Wizara ya Mambo ya  Nje.
Membe alisema kuwa anashangaa na ikiwezekana atapiga marufuku timu za Simba na Yanga kwenda kushiriki mashindano huku akisisitza kuwa DarfuR hakuna hotel kwani  viongozi na baadhi ya mabalozi ambao wanakwenda huko hupokewa kwenye mabasi ambayo hayapitishi risasi ili kuwaweka katika hali ya usalama .

Membe aliongeza kwa kusema atakwenda kuzungumza na mamlaka husika kwanini wamepeleka mashindano huko sehemu ambayo ni hatari kwani kufanya hivyo ni fedheha kwa taifa kupeleka wachezaji sehemu amabayo hakuna usalama kwa sasa .
Timu za Simba na Yanga zitaiwakilsisha Tanzania Bara  katika mashindano hayo yatakayoaaanza hivi karibuni na kama serikali itazuia basi huenda hata Zanzibar inaweza isipeleke timu kutoakana hali ya kiusalama  

No comments:

Post a Comment