Pages

Saturday, June 1, 2013

MOURINHO AWAAGA MASHABIKI LEO HUKU REAL MADRID IKISHINDA 4-2 DHIDI YA OSASUNA

Kocha wa klabu ya Real Madrid Jose Mourinho leo amewaaga rasmi mashabiki wa klabu hiyo kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu wakati Real Madrid walipokuwa wakicheza mechi yao ya mwisho dhidi ya Osasuna.
Mourinho alitumia dakika mbili mara baada ya mpira kuisha kuwaaga mashabiki wa klabu hiyo kwa kuwapungia mkono lakini alipata majibu nusu kwa nusu kwani baadhi ya mashabiki walimzomea lakini wengine walimpigia makofi. 
Hali hii imetokea kutokana na mgongano uliopo kwani baadhi ya washabiki wanaamini Mourinho ameharibu soka la klabu hiyo lakini wengine wanaamini ameleta mafanikio ndani ya klabu hiyo ambayo ilikuwa kwenye hali mbaya wakati anaipokea kutoka kwa Manuel Pellegrini. Baada ya mchezo huu, Mourinho anatarajiwa kuelekea London tayari kuanza kazi ya kuifundisha klabu ya Chelsea baada ya kusaini mkataba wa miaka minne wenye dhamani ya paundi mil 40. 
Katika mchezo wa leo Real Madrid imeweza kushinda kwa magoli 4-2 dhidi ya Osasuna, magoli ya Madrid yamefungwa na Higuain (35), Essien (38), Benzema (69) na Callejo (87).  
Farewell: Mourinho waves goodbye to the fans after the match in Madrid
Mourinho akiwaaga mashabiki wa Madrid bila ya kuwa na sura ya furaha kwani anatambua kuwa wengi wao hawampendi na wanaamini hajaleta mafanikio yoyote ndani ya klabu hiyo


Real Madrid's Portuguese coach Jose Mourinho Real Madrid's coach Jose Mourinho
Kwa huzuni, Mourinho akiwaaga mashabiki wa Madrid

No comments:

Post a Comment