Pages

Tuesday, June 4, 2013

SIMBA, AL HILAL, AL MERREIKH ZAJITOA KUSHIRIKI CECAFA


Nicholas Musonye katibu mkuu wa CECAFAKlabu ya Simba kutoka Tanzania, imetangaza kuwa haitashiriki katika michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa kanda ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA, ikiwa itaandaliwa katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

Uamuzi huo umechukuliwa kufuatia mjadala ulioibuka katika bunge la Tanzania baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Benard Membe kuhoji hali ya Usalama katika eneo hilo.

Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amesema uongozi wa CECAFA ni sharti ubadilishe mahala pa fainali hizo la sivyo wao hawatashiriki.''Hatuwezi kwenda Darfur kuvalia mavazi yasiyopenya risasi'' Alisema Bwana Rage.''Ni wazi kuwa hali ya usalama katika eneo hilo sio nzuri kama ilivyothibitishwa na serikali'' Aliongeza mwenyekiti huyo wa Simba.

Membe aliliambia bunge la Tanzania kuwa alishangazwa sana na uamuzi wa kuandaa fainali hizo katika eneo la Darfur ambalo limekumbwa na mapigano ya mara kwa mara.Membe amesema serikali ya Tanzania, inachunguza hali ilivyo na kuwa watachukua uamuzi muafaka kuhusiana na suala hilo.

''Hatuwezi kuwatuma vijana wetu katika eneo ambalo hatuna hakikisho la Usalama'' Alisema Membe.Mabingwa watetezi Yanga, vile vile kutoka Tanzania ambao walikuwa wameonyesha nia ya kushiriki katika fainali hizo za Darfur, pia nao wanasema watafuata ushauri kutoka kwa serikali.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka la soka nchini Tanzania (TFF),  Angetile Osiah, amesema wao wamehakikishiwa usalama na eneo watakalopiga kambi wakati wa mashindano hayo.

Endapo timu hizo mbili kutoka Tanzania zitajiondoa kutoka kwa fainali hizo, itakuwa pigo kubwa kwa waandalizi wa mashindano hayo.Timu mbili kubwa nchini Sudan Al Hilal na Al Merreikh tayari zimethibitisha kuwa hazitashiriki kutokana na hofu za kiusalama.Katibu mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye amekaririwa akisema kuwa eneo hilo la Darfur ni salama kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment