Pages

Saturday, June 8, 2013

BUYERN MUNICH YAMUONGEZEA FRANK RIBERY MIAKA MIWILI


Winga wa Bayern Munich Franck Ribery amesaini kuongeza mkataba wa miaka miwili na klabu yake hiyo ambao ni mabingwa wa vilabu Ulaya mkataba ambao utamuweka hapo mpaka 2017.

Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka , 30 aliisaidia Munich kuwa timu yan kwanza ya Ujerumani kushinda kwa pamoja mataji matatu ndani ya msimu mmoja yakiwemo mataji ya Bundesliga, European Cup na German Cup.

Mlinzi raia wa Belgium, Daniel Van Buyten mwenye umri wa miaka 35, naye anatarajiwa kusalia hapo kwa mwaka mmoja zaidi.
Bayern ndiyo timu ya kwanza  nchini Ujrumani kutwa mataji mengi yakiwemo ya ligi ya nyumbani na Ulaya ndani msimu mmoja.

Inakuwa ni timu ya saba kufanya hivyo barani Ulaya kama ilivyokuwa kwa Celtic mwaka 1967, Ajax mwaka 1972, PSV Eindhoven mwaka 1988, Manchester United mwaka 1999, Barcelona mwaka 2009 na Inter Milan mwaka 2010.

No comments:

Post a Comment