Pages

Saturday, June 8, 2013

UGANDA YAJIWEKA KWENYE NAFASI NZURI BAADA YA KUIFUNGA LIBERIA 1-0 LEO



Uganda Cranes imejiweka katika nafasi nzuri  leo katika kufuzu kombe la dunia  2014 baada ya kuifunga Liberia bao 1-0 katika Uwanja wa Mandela jijini kampala.
 Mechi hiyo iliiisha vibaya baada ya wachezaji wa Liberia wakiongozwa na nyota wao  Roberts Omega kumzonga mwamuzi wa mchezo Adam Cordier kutoka  Chad kwa kile walichodai kuchezesha vibaya kiasi cha kuwafanya wa kushindwa kuvumulia benchi la  ufundi ilibidi wapunguze hasira ili kutuliza vurugu hizo.

Goli la ushindi liliwapa mashabiki wa Uganda hari ya juu mara baada ya  Tonny Mawejje  kufunga goli katika dakika ya sita ya mchezo, goli lililopatikana baada ya kuidanganya safu ya ulinzi ya  Liberia na kuachia shuti kali huku safu ya ulinzi  isijue cha kufanya.

Uganda kwa sasa ina pointi 5 sawa na Senegal ambao nao wanacheza na  Angola huko  Luanda katika kundi  J. Timu zote zina alama 5 huku Liberia ikiwa na alama 4 wakati  Angola wao wana alama  3.Timu inayoongoza kwa kila kundi itafuzu kwa hatua ya pili ya mtoano.

No comments:

Post a Comment