Pages

Tuesday, June 11, 2013

AMRI KIEMBA AJIFUNGA MIAKA MIWILI SIMBA


Kiungo Amri Ramadhani Kiemba amesaini mkataba  wa miaka miwili na Simba  leo mchana hivyo ataendelea kuichezea klabu hiyo kwa msimu ujao

Akizungumza na Lenzi ya Michezo jioni hii Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang’are ‘Mzee Kinesi’ alisema ni kweli wameshaingia mkataba na mchezaji huyo leo mchana.

Pia nilizungumza na Kiemba wakati akiwa kwenye mazoezi ya timu ya taifa na kukiri kuingia mkataba wa miaka miwili hivyo ataendelea kuwepo Msimbazi

“Mimi kweli nimesaini Simba ila nashangaa magazeti yalikuwa yanatoa wapi habari za mimi kuwa nimesaini Yanga kwani sikuwahi kuongea nayo”, alihoji Kiemba.


Kiemba kwa sasa yupo kambini na timu ya Taifa kujiandaa na mchezo na Ivory Coast utakaochezwa jumapili  hii baada ya mchezo uliopita kufungwa na Morocco mabao 2-1, bao ambalo stars ililipata kupitia kwa Amri Kiemba dakika ya 62.  

No comments:

Post a Comment