VYUO VIKUU MORO KUCHUANA KWENYE POOLTABLE MBELE YA KAMANDA WA POLISI WA MKOA
KAIMU
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, John Laswai leo atakuwa mgeni rasmi katika
mashindano ya mchezo wa pool kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya mkoani hapa ambayo
yanajulikana kama 'Safari Lager Higher Learning Pool Competition 2013'.
Aliongeza kwa kuvitaja vyuo
vitakavyoshiriki mashindano hayo kuwa ni chuo cha SUA, Mzumbe, Ardhi na chuo
cha uandishaji wa habari ( MSJ).
Lugeng'ha alisema kuwa mashindano hayo
yatachezwa kwa mtindo wa chuo kwa chuo na mchezaji mmoja mmoja wanaume na
wanawake.
Alisema bingwa kwa upande wa chuo licha ya
kujinyakulia fedha taslim Sh.500,000 pia itakuwa imekata tiketi ya kuuwakilisha
mkoa huo katika fainali za taifa zitakazofanyika kuanzia Juni mosi mwaka huu
jijini Dar es Salaam, mshindi wa pili atazawadiwa Sh.300,000, mshindi wa tatu
Sh.200,000 na mshindi wa nne Sh.100,000.
Aidha alisema kuwa bingwa kwa upande wa
mchezaji mmoja mmoja (wanaume) atajinyakulia Sh.150,000 na tiketi ya kushiriki
fainali za taifa, mshindi wa pili Sh.100,000, ambapo bingwa kwa upande wa
wanawake atazawadiwa Sh.100,000 na tiketi ya kushiriki fainali za taifa huku
mshindi wa pili akiondoka na Sh.50,000.
Post a Comment