Pages

Friday, May 3, 2013

TAIFA STARS NDOGO NI VITA YA NAMBA, BARTHEZ NAYE HAJALALA AONYESHA UWEZO WAKE

Husein Twaha akipiga pasi kwa Emilly Mgeta huku Miraji Said akimwangalia
Kena Ngoma akipiga mpira huku Husein Javu akijaribu kuuzuia wakati wa mazoezi ya jioni hii

Golikipa Ali Mustafa akidaka mpira kwenye mazoezi ya leo jioni wakati wakicheza mpira wao kwa wao
Barthez akienyeshwa na Kocha wa magolikipa Juma Pondamali

Zahoro Pazi akienyeshana na mchezaji mwenzake

KIPA Ali Mustapha “Barthez” leo alionekana kufanya vizuri kwenye mazoezi ya timu ya Taifa yanayofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam iliyopo  tangu jana.

Barthez ambaye ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Young Stars alikuwa akipangua mashuti ya wachezaji wenzake hali iliyomfanya kocha Kim Poulsen kumpongeza.

Timu hii inajumuisha wachezaji ambao wamepita umri wa kuchezea timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) na wakubwa ambao hawajapata fursa ya kuingia Taifa Stars kocha anaitumia kuangalia uwezo wao.

Akizungumza LENZI YA MICHEZO baada ya mazoezi Meneja wa timu hiyo Tasso Mukebezi amesema kuwa wachezaji wote wapo kambini isipokuwa wachezaji ambao wapo safari nchini Morocco na timu yao ya Azam.

“Wachezaji  wote walioitwa wameingia kambini isipokuwa wachezaji wa Azam ambao wapo nchini Morocco kwa ajili ya mchezo wao na FAR Rabat”, alisema Tasso

Pia alisema watakuwa kambini hadi Mei 6, mwaka huu ili kocha apate nafasi ya kuwaangalia kwa karibu kwani mchezaji anaangaliwa uchezaji uwanjani pia tabia yake anavyojumuika na wenzake.

“Jinsi mchezaji anavyoshirikiana na wenzake nje ya uwanja ndivyo anavyoweza kushirikiana na wenzake uwanjani vitu ambavyo kocha anavizingatia”, alisema Tasso

Wachezaji waliopo kambini ni Hussein Shariff  na Ali Mustapha  ambao ni makipa,  Mabeki ni Ismail Gambo, Kessy Hassan, Kennan Ngoma, Miraji Adam, Mohamed Hussein na Emily Mgeta.

Viungo ni Haruna Chanongo, Edward Christopher, Mudathiri Yahya, William Lucian, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, Jimmy Shoji, Abdallah Seseme, Ramadhan Singano, Farid Mussa na Vicent Barnabas.

Washambuliaji ni Hussein Javu, Jerome Lambele, Zahoro Pazi, Twaha Hussein, Abdallah Karihe na Juma Luizio.
Wachezaji  Himid Mao, Aishi Manula , David Mwantika, Samih Nuhu, Abdallah Seif na Waziri Salum  wa Azam ndio ambao hawajaingia kutokana na kuwa safarini na timu yao.

Kim aliita timu hiyo ni ambayo ni sehemu ya Mpango wa Maendeleo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliozinduliwa Aprili 4 mwaka huu ukilenga kuendeleza wachezaji.

Timu hii ni kiungo kati ya vijana na wakubwa kwani wachezaji wengi ni vijana lakini wakubwa wachache waliopo wamepata fursa ya kuangaliwa uwezo wao.

Timu hii ni changamoto wa wachezaji wa Taifa Stars kuwa wapo wanaosubiri wazembee ili wachukue nafasi zao.


No comments:

Post a Comment