Husein Twaha akipiga pasi kwa Emilly Mgeta huku Miraji Said akimwangalia |
Kena Ngoma akipiga mpira huku Husein Javu akijaribu kuuzuia wakati wa mazoezi ya jioni hii |
Golikipa Ali Mustafa akidaka mpira kwenye mazoezi ya leo jioni wakati wakicheza mpira wao kwa wao |
Barthez akienyeshwa na Kocha wa magolikipa Juma Pondamali |
Zahoro Pazi akienyeshana na mchezaji mwenzake |
KIPA Ali Mustapha
“Barthez” leo alionekana kufanya vizuri kwenye mazoezi ya timu ya Taifa
yanayofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam iliyopo tangu jana.
Barthez
ambaye ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Young Stars alikuwa akipangua
mashuti ya wachezaji wenzake hali iliyomfanya kocha Kim Poulsen kumpongeza.
Timu hii
inajumuisha wachezaji ambao wamepita umri wa kuchezea timu ya Taifa ya vijana
wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) na wakubwa ambao hawajapata
fursa ya kuingia Taifa Stars kocha anaitumia kuangalia uwezo wao.
Akizungumza LENZI YA MICHEZO baada ya mazoezi Meneja wa timu hiyo Tasso Mukebezi amesema kuwa
wachezaji wote wapo kambini isipokuwa wachezaji ambao wapo safari nchini
Morocco na timu yao ya Azam.
Pia alisema
watakuwa kambini hadi Mei 6, mwaka huu ili kocha apate nafasi ya kuwaangalia
kwa karibu kwani mchezaji anaangaliwa uchezaji uwanjani pia tabia yake
anavyojumuika na wenzake.
“Jinsi
mchezaji anavyoshirikiana na wenzake nje ya uwanja ndivyo anavyoweza kushirikiana
na wenzake uwanjani vitu ambavyo kocha anavizingatia”, alisema Tasso
Wachezaji
waliopo kambini ni Hussein Shariff na
Ali Mustapha ambao ni makipa, Mabeki ni Ismail Gambo, Kessy Hassan, Kennan
Ngoma, Miraji Adam, Mohamed Hussein na Emily Mgeta.
Viungo ni
Haruna Chanongo, Edward Christopher, Mudathiri Yahya, William Lucian, Jonas
Mkude, Hassan Dilunga, Jimmy Shoji, Abdallah Seseme, Ramadhan Singano, Farid
Mussa na Vicent Barnabas.
Wachezaji Himid Mao, Aishi Manula , David Mwantika, Samih Nuhu, Abdallah Seif na Waziri Salum
wa Azam ndio ambao hawajaingia kutokana na kuwa safarini na timu yao.
Kim aliita timu
hiyo ni ambayo ni sehemu ya Mpango wa Maendeleo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) uliozinduliwa Aprili 4 mwaka huu ukilenga kuendeleza wachezaji.
Timu hii ni
kiungo kati ya vijana na wakubwa kwani wachezaji wengi ni vijana lakini wakubwa
wachache waliopo wamepata fursa ya kuangaliwa uwezo wao.
Timu hii ni
changamoto wa wachezaji wa Taifa Stars kuwa wapo wanaosubiri wazembee ili
wachukue nafasi zao.
No comments:
Post a Comment