Pages

Thursday, May 23, 2013

TAIFA STARS MCHANA WAITWA IKULU KUTETA NA RAIS

TIMU ya Taifa 'Taifa stars" ambayo ipo kambini kujiandaa na mchezo wa marudiano na Morocco wa kutafuta kufuzu fainali za dunia 2014 nchini Brazil imealikwa Ikulu kula chakula cha mchana leo.

Taarifa ambazo Lenzi ya Michezo imezipata zinasema Taifa stars imeitwa na Rais leo mchana kula chakula cha mchana paamoja na mambo mengine ambayo yatafahamika baadae.

Stars asubuhi imefanya mazoezi kwenye uwanja wa Karume ikiwa na wachezaji 21 kwani Mwinyi Kazimoto aliumia mguu na Salum Abubakar amefiwa na baba yake mlezi hivyo amekwenda kuhudhuria msiba huo



No comments:

Post a Comment