Pages

Wednesday, May 22, 2013

MICHO KUKAA BENCHI NA SAM TIMBE UGANDA



Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda  Milutin “Micho” Sredojević amechaguliwa kuwa mkufunzi mpya wa timu ya taifa ya Uganda akiziba nafasi ya  Bobby Williamson ambaye aliachishwa kazi  mwezi jana

Micho ambaye ni raia wa  Serbia amechaguliwa jana katika makao makuu ya Shirikisho la soka la Uganda  (Fufa House) huko Mengo, kilometa chache kutoka  jiji la  Kampala na ametia saini kandarasi ya miaka miwili .

Williamson aliiongoza Uganda Cranes kushinda mara nne kombe la baraza la vyama vya soka la Afrika Mashariki na Kati  Challenge Cup lakini alishindwa kuipeleka ti mu hiyo katika mashindano ya mataifa ya afrika .

Aidha  Micho amesema na akitumia Lugha ya kiganda kwa lafudhi mbaya "  Luganda ,  “Nasikia heshima sana na kujivunia kupewa kuifundisha timu ya taifa ya Uganda ambayo aliiondoka Uganda 2004, nilikuwa sipo kimwili lakini roho yangu ilikuwa hapa na inapendeza sana kurudi hapa. Na nina imani kuipeleka nchi mbali zaidi ” 

Micho, 43, atasaidiwa na kocha wa timu ya  polisi ya uganda  Sam Timbe, na kocha wa Bul Bidco  Kefa Kisala na  kipa wa makocha  Fred Kajoba.
Aidha kocha huyo amewahi kufundisha timu za St.George of Ethiopia, South Africa’s Orlando Pirates pia  Al Hilal ya Sudan

No comments:

Post a Comment