Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 13, 2013

SUREBOY AKATAA MILIONI 50 ZA YANGA



KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Abubakari Salum ‘SureBoy’ amekataa ofa ya mshahara Sh milioni mbili iliyotolewa na Yanga ili waweze kupata saini yake.

Yanga ambao wanahitaji saini ya kiungo huyo, walikuwa tayari kumpa Sh milioni 50, ikiwa ni dau la usajili wake wa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mabingwa hao wa ligi hiyo, ambao walikuwa na nia ya kumchukua kiungo huyo, wanaweza kumkosa baada ya kumahidi kulipwa mshahara wa Sh milioni mbili anaolipwa na klabu yake ya Azam FC.

 Habari zilizopatikana Dar es Salaam jana, kutoka ndani ya klabu hiyo, zilieleza kwamba kiungo huyo ameshindwa kushawishika na fedha ambazo walipanga kumpa.
Chanzo hicho kilieleza kwamba kiungo huyo, anaona kiasi alichotengewa ni kidogo kwani fedha hizo ndizo anazolipwa katika klabu yake ya Azam.

Kilieleza kwamba, Yanga wangepandisha dau angeweza kukubali kuondoka Azam FC kutokana na mkataba wake unatarajia kumalizika Desemba mwaka huu.
“Yanga ilikuwa inamhitaji Sureboy lakini amekataa kutokana na kutoshawishika na kiasi alichotajiwa,” kilieleza chanzo chetu.

Chanzo hicho kilieleza kwamba, sababu nyingine iliyomfanya akatae kujiunga na Yanga ni baada ya Kocha Mkuu wa Azam FC, kumhakikishia kuwa atamwongezea mkataba mpya.
Kilieleza kwamba, kiungo huyo, ameona ni bora abaki Azam FC, ambaye ameahidiwa kulipwa donge nono baada ya mkataba wake wa awali kumalizika kuliko kwenda Yanga kwa dau la Sh Milioni 50.

No comments:

Post a Comment