Pages

Wednesday, May 22, 2013

SIMBA WAHAHA KUSAKA SAINI YA NIYONZIMA


SIMBA inahaha kwa nguvu zote kusaka saini ya kiungo fundi wa Yanga, Haruna Niyonzima, lakini kauli ya staa huyo wa Amavubi inazima ndoto zote za wababe hao wa Msimbazi baada ya kusema: "Sitaki kuendelea kusota hapa nchini."
Vuguvugu la usajili wa Tanzania Bara limeshaanza chini kwa chini, huku Simba ikitaka kumnasa kiungo huyo ambaye hadi sasa hajamwaga wino wa kuendelea kuichezea Yanga baada ya mkataba wake kuripotiwa kumalizika mwisho wa msimu huu.
Uongozi wa Yanga, unapambana kumbakiza nyota wao huyo, lakini tatizo lililopo kwa sasa ni makubaliano ya maslahi ambayo anataka kuhakikishiwa kabla ya kuanguka saini itakayomfanya abaki kwenye timu.
Niyonzima aliiambia Lenzi ya Michezo kwamba kwa sasa ligi imekwisha na anafurahia timu yake ya Yanga kutwaa ubingwa, lakini hilo halimfanyi kuwa na furaha kubwa kwasababu amechoka soka la Tanzania.
Kiungo huyo alisema kwamba sasa hafikirii kusaini katika klabu yoyote ya hapa nchini kwani ndoto zake ni kucheza soka nje ya Bara la Afrika.
Lakini, LENZI YA MICHEZO  lilipata ripoti kwamba kiungo huyo aliwahi kuketi na baadhi ya mabosi wa Simba kuzungumza juu ya kuinasa saini yake ili msimu ujao aitumikie timu hiyo ya Msimbazi.
Lakini, Niyonzima mwenyewe alibainisha hivi karibuni kwamba anataka kucheza timu ambayo itashiriki michuano ya kimataifa ili iweze kumpa fursa ya kuonekana na timu za nje.
Kwa mahitaji hayo ya Niyonzima, tayari Simba itakuwa imeshindwa kufuzu masharti yake kwa kuwa msimu ujao timu hiyo inayonolewa na Mfaransa Patrick Liewig, haitashiriki michuano yoyote ya kimataifa.
Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako, akizungumzia suala la mchezaji huyo na kudai kwamba huu si wakati mwafaka kwa kuwa bado kuna mambo mengi wanatarajia kuyafanya.
Aliwataka wapenzi wa Yanga kuendelea kusherehekea ubingwa wa timu yao, huku wakiwa na imani kuwa uongozi wao utafanya usajili mzuri utakaoiwezesha timu yao kufanya vizuri katika michuano ya Ligi Kuu msimu ujao na vilevile michuano ya kimataifa

No comments:

Post a Comment